Home Kitaifa RC SENDIGA AAGIZA MIUNDOMBINU YA SHULE YA MANYARA ‘GIRLS’ KUKAMILISHWA

RC SENDIGA AAGIZA MIUNDOMBINU YA SHULE YA MANYARA ‘GIRLS’ KUKAMILISHWA

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Agosti 14, 2024, ametembelea Shule ya mpya wasichana ya Manyara Girls na kuongea na wanafunzi pamoja na kuwakaribisha rasmi Mkoa wa Manyara wanafunzi 110 waliokwishawasili shuleni hapo na kuanza masomo yao ya kidato cha tano (5) kwa mchepuo wa Sayansi (PCM na PCB).

Mhe. Mkuu wa Mkoa, amewashukuru na kuwapongeza wazazi walioleta watoto wao katika shule hiyo mpya na kuwahakikishia watoto wao watapata Elimu na huduma bora, ulinzi na usalama wakati wote watakapo kuwepo shuleni hapo.

Sambaba na hilo RC Sendiga, ameagiza umaliziaji wa miundombinu yote ambayo bado haijakamilika ikamilike mapema ili wanafunzi waweze kupata huduma hizo hasa ya bwalo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!