Home Kitaifa TANZANIA TUNA ZIADA YA MCHELE TANI MILIONI 1.6 – BARAZA LA MCHELE

TANZANIA TUNA ZIADA YA MCHELE TANI MILIONI 1.6 – BARAZA LA MCHELE

Tanzania tuna ziiada ya Mchele tani zaidi ya milioni 1.6 baada ya kujitosheleza mahitaji ya nchi kwa chakula kwamujibu wa takwimu za uzalishaji wa Mchele wa msimu wa mwaka 2023/24.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mchele Tanzania RCT Geoffrey Rwiza wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dar es salaam amesema katika msimu wa mwaka 2022/23 ltaifa lilikuwa na ziada ya Mchele tani laki Saba na nusu ambayo ziada ya Mchele ni fulsa kibiashara sio kero.

Amesema kwasasa wakulima wa Tanzania tunaozalisha ziada baada ya serikali kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya kilimo kwa zao la mchele kwa ujumla ambayo imesaidia mabadiliko ya kuongeza uzalishaji wa mchele nchini.

Rwiza alisema pia kwa sasa taifa limekuwa likipata fedha za kigeni kwa kiwango cha juu katika sekta ya kilimo kupitia zao la mchele “Sasa zao la mchele lunaongoza kuingiza nchini fedha za kigeni kutokakana na zaidi ya kiwango cha akiba ya zao Hilo”

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo wa Baraza la Mchele Tanzania ameomba Halmashauri nchini kutoza ushuru wa mchele kwa wafanyabiashara wa mchele sio wakulima wa mpunga nchini kwani Wakulima huishiwa mitaji wakati wa kilimo hivyo kuendelea kumtoza ushuru ni kumbebesha gharama zinazopelekea mkulima kuingia kwenye mikopo inayomkwamisha baadae.

“Huu ushuru kwa Halmashauri ni muhimu na upo kisheria na uliwekwa kwaajili ya mfanyabiashara sio mkulima lakini kwasasa anatozwa mkulima wakati anatoa mazao yake shambani akiwa ameishiwa hela hivyo hulazimika kukopa ili walipe Halmashauri kabla hawajauza kwakuwa anakuwa ameishiwa kweli kweli ” alisema Rwiza.

“Kama ushuru kwa mkulima kwanini tusisubiri wakati anauza badala ya kumtoza ushuru wakati akiwa amechoka kweli kweli kwa gharama za kilimo”

Lakini pia Rwiza ameomba ulinganifu wa kiwango cha utozaji ushuru kwa Kila halmshauri nchini ilikusiwe na tofauti ya bei ya Mchele kwasababu ya utofauti wa tozo za ushuru wa Halmashauri nchini ambayo hupelekea maeneo mengine kuwa na bei kubwa ya Mchele na kwimgine bei ndogo.

“Lakini tunahisi kwa kukiwa na ulinganifu wa viwango vya ushuru itasaidia kupunguza bei ya mchele.nchini na kuwapunguzia gharama za kilimo mkulima nchini” alisema Rwiza.

Akizungumzia kuhusu Serikali’ kujiunga na majukwaa la kilimo endelevu cha mpunga duniani Rwiza ameomba Serikali’ irithie kujiunga na Jukwaa la kilimo endelevu cha mpunga duniani ili taifa letu nalo liweze kunufaika na kufaidi matunda ya tafiiti za sekta mchele duniani.

Hatahivyo akizungumzia suala la mikopo kwa Wakulima wa mpunga Rwiza ameomba Serikali’ ibadilishe sera ya mikopo kwa Wakulima wa mpunga nchini kwa kuweka viwango vya riba inayoshabihiana na mapato ya kilimo cha mpunga na muda wa kulipa mikopo hiyo kwani wao huwa wanasubiria bei kupanda baada ya mavuno hivyo mkulima kurejesha deni katika kipindi cha baada ya mavuno huwa ni ngumu.

“Serikali iangalie upya sera ya fedha ya banki kuu kwani sio rafiki kwa Wakulima wa mpunga kukopesheka hivyo banki kuu iandae sera mahususi kwaajili ya Wakulima wa mpunga kukopesheka.

“Kwa kweli Wakulima wa mpunga wanakuwa na changamoto za kifedha za kuhudumia mashamba yao lakini sera ya mikopo hazijawa rafiki kwao ingawa baada ya mauzo wanakuwa na uwezo wa kurejesha mikopo yao”
++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!