Wachimbaji Madini Mkoa wa Dar es salaam na Mkoa Pwani Wametakiwa kuhamasisha wanamaliza manung’uniko na malalamiko ya Wananchi dhidi yao kabla ya kipindi cha chaguzi kinachotarajia kuanza mwishoni mwa mwaka huu ili isijekuwa kikwazo cha ushindi kwa Wagombea.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo ndg. Abdulsharifu Zahoro wakati akifungua Katika kikao cha kawaida cha viongozi wa chama cha wachimbaji wa madini Mkoa wa Dar es salaam na Pwani (DACOREMA) akimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete.
Alisema wamekuwa wakikutana na manung’uniko na malalamiko ya Wananchi dhidi ya Wachimbaji wadogo wa madini katika vijiji hivyo yashushhulikiwe mapema kabla ya kufika katika kipindi cha chaguzi yakawakwamisha Wagombea.
Mwenyekiti wa wachimbaji wa madini Dar es salaam na Pwani Josephat Mchombamcheka amesisitiza kila anaetaka leseni ya uchimbaji wa madini mkoa wa Dar es salaam na Pwani inatakiwa ajiunge na na chama Cha DACOREMA ili kurahisisha kuwatambua.
Kwa upande wake Afisa Madini Mkazi Dar es salaam na Pwani Lameck Masanja amesema shilingi Bililoni 1.7 zimekusanywa katika mwaka wa fedha wa 2023/24 kiasi ambacho hakikuwahi kukusanywa hapo awali.
Aidha amewataka wachimbaji kuacha kujaza uzito uliopitiliza maalufu kama LUMBESA na iwapo watashindwa kutekeleza hilo wataweza kufungiwa Leseni zao.