Home Kitaifa WAZIRI DKT JAFO; ATOA MAELEKEZO KWA SIDO KUSHIRIKINA NA KILA MKOA UJENZI...

WAZIRI DKT JAFO; ATOA MAELEKEZO KWA SIDO KUSHIRIKINA NA KILA MKOA UJENZI WA VIWANDA VIDOGO 20 KWA MIAKA 6

Na Magrethy Katengu–Dar es salaam

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Selemani Jafo ameliagiza Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kushirikiana na kila Mkoa katika mikakati uwekezaji wa viawanda 3 vikubwa vidogo 20 na vya kati 5 kulingana na malighafi inayozalishwa illi kufanikisha Mpango mkakati wa mika 6 utakaoanzia 2025 utakachochea kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira Nchini.

Agizo hilo amelitoa leo Agosti 9,2024 katika ziara yake alipotembelea Makao makuu Sido Jijini Dar es salaam ambapo amesema Sido Tanzania vijana wengi wanaohitimu vyuo vikuu ni wastani wa vijana elfu sitini na nne kila mwaka idadi hiyo ni kubwa na hapo hatujaangalia vyuo vya kati na Serikali haiwezi kuajiri vijana wote hao wataajiriwa kwenye viwanda au biashara hivyo lazima mikamati thabiti iwekwe ili kunusuru tatizo la ajira.

“Nimeagiza wataalamu kuweka mkakati wa mpango wa mika 6 huu ambao nyinyi kama Sido lazima mshirikiane na muangalie katika viwanda hivyo vidogo 20 mtekeleze hilo kwani kufanya hivyo ni kutatua tatizo la ajira kwani Viwanda vinachukua idadi kubwa ya watu wengi na kuwaajiri ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi na haichagu walio na elimu kubwa na wasio na elimu inayegemeana na kazi atakayoenda kufanya kulingana na uhitaji ikiwemo. watoa huduma ikiwemo Usafiri, huduma.za kifedha, vyakula ” amesema Waziri Dkt Jafo

Waziri Dkt Jafo amewaomba wafanyakazi wote wa SIDO kushirikiana kuwa na upendo katika utendaji wao ili kusaidia kutimiza malengo waliyojiwekea .

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Sido Mhandisi Prof Sylvester Mpanduji ameshukuru ujio wa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Selemani Jafo hivyo maelekezo yote aliyoyatoa ya ujenzi wa viwanda vidogo 20 wao kwakuwa wanahusika na utoaji wa mafunzo ya teknolojia na hivyo watatekeleza hilo kwakuwa wanashirikiana na benki mbalimbali ikiwemo Azania CRDB kwa kuwadhamini wale wote wenye nia ya kuwekeza viwanda kwakuwa kuwadhamini ili wafanikiwe programu hiyo wamekuwa wakiiendesha muda mrefu

” Niwahakikishie Umma kuwa Sido tupo Mikoa yote Tanzania bara huduma zetu zimelenga kwenda kuwasaidia kutoa huduma za kiteknolojia, mafunzo namna ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo nasisi tuna karakana zetu za kuchakata mazao ya mifugo na misitu

Hivyo unaweza ukawa na maarifa lakini huna fedha hivyo mfuko wetu uwezo wake ni milioni 5 hivyo tumeshirikiana na CRDB na Azania benki ambapo mjasriamali mwenye kiwanda anauwezo wa kukopeshwa zaidi ya milioni tano kwa riba nafuu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!