Home Kitaifa TUZO ZA TAMTHILIA ZA KIMATAIFA KUZINDULIWA AGOSTI 24,2024

TUZO ZA TAMTHILIA ZA KIMATAIFA KUZINDULIWA AGOSTI 24,2024

Na Magrethy Katengu-Dar es salaam

WASANII filamu za Bongomovie wameshauriwa kuchangamkia fursa waliyopewa Kimataifa kupitia Tuzo za Tamthilia zinazotarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 24,2024 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari leo Jijini Dar es salaam Agosti 07,2024 Meneja wa Kitengo cha Uhakiki kutoka Bodi ya Filamu nchini Boppe Kyungu amesema Serikali kupitia Bodi ya Filamu inazitambua tuzo hizo,ambapo pamoja na mambo mengine amewaomba wadau wa Filamu nchini Kuungana ili kusaidia kuzifanikisha tuzo hizo kwani ni nyenzo ya kuboresha Sekta ya Filamu ya Michezo ya Kuigiza nchini.

Hata hivyo Kyungu amebainisha kuwa Wadau wa Filamu wachangamkie Fursa hiyo Kwani tuzo hizo zinaenda kuacha alama na kuona kasi mpya ya kutengeneza kazi zenye ushindani Kimataifa pamoja na kutangaza utalii na Utamaduni kupitia sekta ya Filamu nchini.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa Tuzo za Tamthilia nchini Eliya Mjata amesema ujio wa tuzo hizo zinalenga kutoa fursa na wigo mpana kwa wasanii kuipa heshima tasnia na nafasi kwa watayarishaji wa Kazi za Sanaa ambao kwa sasa Wanachukua Nafasi kubwa kuchangia pato la taifa na kukuza Utamaduni na Kutangaza Utalii na lugha ya Kiswahili kupitia kazi zao.

Sambamba na hayo amesema kuwa kumekuwepo tuzo mbalimbali ambazo zinaandaliwa akizitaja Tuzo za Filamu zinazoandaliwa na Bodi ya filamu,Tuzo za Muziki chini ya Uongozi wa Baraza la Sanaa taifa(BASATA) lakini kumekuwepo changamoto ya eneo la Tamthilia kutopewa Nafasi kubwa zaidi.

Mjata amesema Tuzo hizo za Filamu ambazo zinaonyeshwa kwenye kupitia vyombo mbalimbali vya habari zitashirikisha Watayarishaji, Wasanii,Wadau wengine kutoka nchi mbalimbali duniani.

“Tunapenda Kuishukuru Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo tulifanya kikao nao nakuomba mambo kadhaa yakiwemo kutafuta fursa kama programu za kubadilishana uzoefu katika nchi mbalimbali i16 kiwemo Uturuki, China,Japan,Marekani, India,Pakistan, Ufaransa, Ujerumani, Ufilipino na Uingereza.”

Nae Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Idara ya Diplomasia na Uchumi Maryam Vuai amesema Mambo yaliyotumwa na Waandaaji wa Tuzo hizo yamefika Wizarani na watahakikisha wanatoa Ushirikiano Mkubwa kupitia Sekta ya Filamu.

Vuai ameongeza kuwa Wizara inategemea kupitia tuzo hizo zitaweza kubadilishana uzoefu na Utamaduni kupitia nchi shiriki pamoja na Kukuza Lugha ya Kiswahili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!