Home Kitaifa TIA -KUFUNGUA TAWI JIPYA MKOA WA TANGA

TIA -KUFUNGUA TAWI JIPYA MKOA WA TANGA

Na Monica Sibanda – dodoma

Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA inatarajia kufungua tawi lao kubwa Tanga ambalo wanategemea kwamba litakua linafundisha wanafunzi kwanzia level mbalimbali.

Hayo yamebainishwa jana Agosti 7 2024 na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa William Pallangyo alipotembelea banda hilo lililopo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayoendelea Viwanja vya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

Profesa Pallangyo akizungumzia kuhusu kufungua tawi kubwa la TIA Mkoa wa Tanga amesema ni kati ya mikoa ambayo mda mrefu imekua haina taasisi za elimu ya juu zaidi ungekuta na chuo kikuu huria

Amesema level watakazozitoa ni pamoja na cheti (basic certificate) na Diploma (stashahada) na serikali imewaruhusu kuanzisha shahada za udhamiri katika campus yao ya Singida, hivyo wananchi walioko karibu na kanda ya kati na maeneo mengine.

Sambamba na hayo wanatarajia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa tatu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) unaoitwa “The third international conference on business studies”‘ ambao utafanyika Jijini Arusha.

Amesema wapo kwenye maonesho hayo kwaajili ya kutoa fursa ya elimu kwa wananchi kujua taasisi hiyo majukumu yake pamoja na ushauri wa kitaalamu kwenye haya Maeneo,lakini hasa tumekua wakisaidia wakulima,wavuvi na wafugaji kwenye maswala yahusianayo na uhasibu kama kuweka kuweka kumbukumbu zao za kifedha,kufanya biashara kwa njia sahihi l kuweza kupata masoko ya mazao

“Mkutano huu tumekua tunafanya kila mwaka, mwaka huu tuna tunategemea lifanyike Novemba 7 hadi 9 na mgeni rasmi tunategemea awe ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Biteko atatuongoza kwenye mkutano huo ambao utakua na watu wengi na tutakua na washiriki kutoka sehemu mbalimbali za dunia,”amesema.

Pia Profesa Pallangyo amesema taasisi yao imekuwa ikiona changamoto mbalimbali zinawakabili wanafunzi wanazipata hasa za kulipia ada, kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamepata bahati ya kusoma sekondari lakini wanapofika vyuo vikuu wanapata changamoto za kulipa ada.

Ameeleza kuwa kwa kutambua hilo TIA Taasisi waneaanda “TIA MARATHON ” ikiwa lengo makubwa mawili ikiwemo kundi la kwanza ni kusaidia wanafunzi ambao hawana uwezo wa kifedha.

“Kundi la pili tunawaita “young mothers” Wale wanafunzi ambao wamekuja chuoni lakini pia wana familia , wana watoto wadogo kwa hiyo ili ni kundi ambalo tumeona ni muhimu liweze kusaidiwa kuweza kusoma kwa furaha kwa maana ya kuwasaidia sehemu ya fedha ambazo watazihitaji,”ameeleza.

Ameongeza kuwa kwenye TIA MARATHON wanatarajia kufanya Oktoba 26 mwaka huu na mgeni rasmi ni Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!