Na Shomari Binda-Musoma
Mbunge wa jimbo Musoma mjini Vedastus Mathayo ameendelea na ziara ya kukutana na viongozi wa CCM wa matawi na Kata kuhamasisha ushiriki wa uchaguzi serikali za mitaa.
Leo agosti 5 ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake amewatembelea viongozi hao kwenye Kata ya Iringo na Kitaji baada ya jana kuwafikia Kata ya Mukendo na Mwigobero.
Kwa yakati tofauti akizungumza na viongozi hao mbunge Mathayo amesisitiza kupendana kwanza kwa viongozi hao kisha upendo huo kuususha kwa wanachama na wananchi.
Amesema sio vyema kwa viongozi kusemana pembeni bali vipo vikao na maeneo maalum ya viongozi kuzungumza.
Mathayo amesema kiongozi apaswi kumdharau kiongozi mernzake kutokana na nafasi aliyonayo kwa kuwa ndani ya CCM hata kiongozi wa juu anmuheshimu kiongozi wa tawi.
” Ndugu zangu viongozi nimewapitia kufanya uhamasishaji kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao upo mbele yetu.
” Tunakwenda kuhamasisha wanachama na wananchi lakini sisi kwanza tuwe na upendo tunapokwenda kufanya kazi hii”,amesema Matahayo.
Baadhi ya viongozi wa CCM walioshiriki vikao hivyo vya mbunge wamempongeza kwa kuwakutanisha na kusisitiza upendo kabla ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi.
Awali mapema asubuhi mbunge huyo wa jimbo la Musoma mjini amefika ofisi za Tanesco kutaka kujua lini utaratibu wa kumalizia kuwafikishia umeme wa REA wananchi wa pembezoni ukiwemo mtaa wa Songambele.