Home Kitaifa TAKUKURU MARA YASAIDIA TRA KUKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 79 KWA MIEZI 3

TAKUKURU MARA YASAIDIA TRA KUKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 79 KWA MIEZI 3

Na Shomari Binda-Musoma

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU )mkoa wa Mara imesaidia Mamlaka ya Mapato ( TRA ) Mara kukusanya kiasi cha shilingi milioni 79,170,716,00 kwa kipindi cha mwezi aprili hadi juni kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Fedha hizi zimekusanywa katika halmashauri 2 za mkoa wa Mara ambapo wilaya ya Rorya kiasi cha milioni 66,642,605,00 kimekusanywa na milioni 12,527,111,00 kimekusanywa wilayani Butiama kwa kipindi hicho.

Makusanyo hayo yametokana na kazi ya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya zuio kupitia maazimio yaliyofikiwa.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mara Antony Gang’ola ameyasema hayo leo agosti 5 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi aprili hadi juni 2024.

Amesema uchambuzi wa mfumo uliofanywa na taasisi hiyo kwa wilaya ya Rorya na Butiama ulibsini mapungufu mbalimbali ikiwemo TRA kutokukusanya kodi hiyo ya zuio,uelewa mdogo wa wafanyabiashara kuhusu kodi ya zuio na baadhi ya watoa huduma kutokuwa na namba ya mlipa kodi.

Naibu Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema katika kipindi hicho wamefanya uchambuzi wa mfumo katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii ( TASAF) katika Kijiji cha Songolo wilayani Butiama na kubaini kuwepo jina la marehemu kwenye orodha ya wanufaika wa TASAF na fedha kuendelea kupokewa na ndugu wa marehemu.

Amesema kufuatilia eneo hilo tayari mratibu wa TASAF wilaya ya Butiama ametuma jina hilo makao makuu ili liondolewe kwenye orodha.

“Takukuru Mara inaendelea kuteeleza majukumu yake na mafanikio makubwa yameedelea kupatikana na kuokoa fedha za serikali.

” Katika kipindi hiki cha miezi 3 miradi 30 yenye thamani ya shilingi bilioni 13,597,610.00 ikiwemo ya afya,elimu,maji na barabara imefatiliwa”,amesema.

Golong’a amesema miradi 3 yenye thamani ya shilingi milioni 897,184,457.00 kati ya hiyo imekutwa na dosari na hatua zimechukuliwa ambazo zimeonekana kuleta mafanikio.

Katika kipindi cha mwaka 2024/2025 Takukuru mkoa wa Mara imejikita katika utoaji elimu ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na kutoa wito kwa wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na kuepukana na vitendo vya Rushwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!