Home Kitaifa YANGA TAWI LA MUSOMA WACHANGIA DAMU NA KUTOA MSAADA HOSPITALI YA MANISPAA...

YANGA TAWI LA MUSOMA WACHANGIA DAMU NA KUTOA MSAADA HOSPITALI YA MANISPAA YA MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

WANACHAMA na mashabiki wa timu ya Yanga kwa kushirikiana na benki ya NBC tawi la Musoma wamechangia damu na kutoa msaada kwenye hospital ya manispaa ya Musoma.

Uchangiaji huo wa damu na msaada wa maji,juice,sabuni na mafuta kwa wagonjwa umetolewa leo agosti 1 ikiwa ni kueleekea siku ya wananchi agosti 4.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya tukio hilo Mwenyekiti wa Yanga tawi la Musoma na mratibu wa mkoa wa Mara Ismail Massaro amesema huo ni utaratibu wanao ufanya kila mwaka.

Amesema Yanga haiwezi kupishana na jamii na kila mwaka kabla ya kuanza msimu wa ligi wanafanya tendo la huruma kwa jamii.

Massaro amesema mwaka jana kabla ya msimu kuanza walitembelea vituo vya watoto wanao ishi kwenye mazingira magumu na mwaka huu wameona watembelee hospital ya manispaa ya Musoma.

” Niwashukuru wanachama na mashabiki wa Yanga tawi la Musoma kwa michango yao na kuweza kufanikisha jambo hili.

” Lakini pia nishukuru benki ya NBC tawi la Musoma kuwa sehemu ya wachangiaji wa kuweza kufanikisha tukio hili adhimu lililofanyika leo”,amesema.

Akizungumzia kikosi chao cha msimu huu mmoja wa wanachama wa Yanga tawi la Musoma Melvin Nashon amesema wanao uhakika wa kuendelea kufanya vizuri kwa kuwa wanacho kikosi bora.

Mganga mfawidhi wa hospital ya manispaa ya Musoma Dk. Emanuel Shani amewashukuru wanachama na mashabiki wa Yanga tawi la Musoma kwa tendo la faraja walilolifanya.

Amesema makundi mengine kwenye jamii yanapaswa kujitolea kusaidia makundi ya wenye uhitaji kwenye maeneo wanayoishi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!