Home Kitaifa TAMASHA LA BATA MSITUNI KUFANYIKA KAZIMZUMBWI

TAMASHA LA BATA MSITUNI KUFANYIKA KAZIMZUMBWI

Na Magrethy Katengu-Pwani

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti atoa taarifa kuwa wanatarajiwa kuwa na Tamasha Kubwa la Kimataifa linalojulikana kama “BATA MSITUNI” litakalofanyika Pugu Kazimzumbwi wilayani humo, mkoani Pwani.

Ayasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Julai 29, 2024 katika eneo la utalii lenye msitu mnene na baadhi ya viumbe ambavo ni vya kipwkee ikiwemo panzi mwenye rangi ya bendera ya Tanzani Pugu Kazimzumbwi wilayani Kisarawe , mkoani Pwani Tamasha hilo litaanza Septemba 3 hadi 9 mwaka huu ambapo nchi zaidi ya tatu (3) zitashiriki ikiwemo Uganda Afrika kusini na Tanzania yenyewe

“Pugu Kazimzumbwi ni moja ya eneo la msitu mkubwa wenye hekari zaidi ya 8000, na eneo hili ni mahususi kwa ajili ya utalii na wa na sisi watu wa Pwani tuna eneo ambalo watu wanaweza kuja kupata faraja,mapumziko wakiwa na familia kupata upepo wa asili, hivyo ni vizuri kubadilishana nao mawazo kupitia tamasha hili la siku 7 tunatangaza tamasha linaitwa “BATA MSITUNI”, hili ni tukio la Kimataifa ambalo halijawahi kufanyika nchini,” amesisitiza DC Magoti

DC Magori amesema tamasha hilo kutakuwa na mashindano ikiwemo ya kupandisha mlima, kuendesha pikipiki,baiskeli,kupiga mbizi kwa kutumia maboti ndani ya bwawa la Usharoba lililomo humo ndani pia kutakuwa na wanamziki mbalimbali watakaotoa burudani hivyo ndiyo maana ni Bata msituni kutafuta pesa na kupata muda wa kuburudika

DC Magoti ameeleza kuwa pamoja na hayo tamasha hilo litatumika kuonesha utamaduni wa Wazaramo katika Wilaya ya Kisarawe na kwamba watakuwa wakitoa burudani kupitia ngoma zao za asili ikiwemo mdogoli.

Ni kwanini wamaliita Tamasha hilo “BATA MSTITUNI”, DC Magoti amesema Bata Msituni ni sehemu yenye uoto wa asili ambayo wamebarikiwa kama inavyofahamika kuwa Tanzania ni nchi yenye misitu mikubwa.

Kisarawe imebarikiwa kuwa na eneo la Pugu Kazimzumbwi la utalii lenye zaidi ya Hekta 8000 ambalo limebarikiwa kuwa na vivutio hivyo wanatengeneza mazingira mazuri ya watalii kwa kujenga hosteli za kisasa ndani ya eneo hilo.

“Ni imani yangu kuwa Mwenyezi Mungu akitupa.pumzi ya uhai tarehe 25 mwezi wa Nane maandalizi yatakuwa yamekamilika, kuna sehemu za VIP ambazo tunazijenga katika hali ya uasili, tofauti watu walizoea kulala kwenye mahoteli makubwa yenye viyoyozi, huku unalala kwenye Lodge nzuri, lakini na kupata upepo mzuri kabisa” amesema DC

Aidha Rais Dkt. Samia Sukuhu Hassan alivyotangaza utalii kupitia The Royal Tour, Kisarawe wameamua kuunga mkono hatua hiyo kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuenedeleza na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!