Home Kitaifa BASHUNGWA ABAINISHA HATUA ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BARABARA NA MADARAJA MKOA...

BASHUNGWA ABAINISHA HATUA ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BARABARA NA MADARAJA MKOA KAGERA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amebainisha hatua za utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Ujenzi inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Kagera hususan ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja.

Bashungwa ameeleza hayo Wilayani Muleba Mkoani Kagera katika Ibada ya Shukrani ya Miaka 12 ya Uchungaji wa Askofu Grayson Mutegeki Katunzi pamoja na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa Anglikana Mt. Yohana Kimbugu, iliyoambatana na Ibada maalum ya kuwaombea Viongozi wa Kitaifa na Serikali.

Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inaendelea na upanuzi kwa njia nne barabara ya Rwamishenyi hadi Bandari ya Bukoba ambapo sasa Mkandarasi anendelea na ujenzi sehemu ya Rwamishenye Round about – Hamugembe hadi stendi ya Bukoba mjini kwa gharama ya Shilingi Bilioni 10.3 ambapo kazi imefikia asilimia 40.

“Katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuwezesha fedha tunaendelea na ujenzi wa njia nne kuanzia Rwamishenye Round about kupitia Kwenye daraja la Kanoni hadi Stendi ya Bukoba Mjini na wakati tunakamilisha, tumepanga kujenga njia nne kuanzia Rwamishenye hadi stendi mpya ya Kyakailabwa” amesema Bashungwa.

Bashungwa amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Karagwe – Benako kwa kiwango cha lami, sehemu ya Bugene-Burigi Chato (km 60), Mkandarasi anaendelea na kazi ambayo imefikia asilimia 41 ya utekelezaji.

Aidha, Waziri Bashungwa amesema Makandarasi wanaendelea na ukarabati wa barabara ya Lusahunga- Rusumo (km 92) kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 153.6.

Amesema Serikali imeendelea na manunuzi ya kupata Makandarasi wa ujenzi wa barabara ya Kyaka- Katoro – Kanazi – kyetema, kipande cha Kanazi-Kalonge (km 10).

Vile vile, Amesema Serikali inakamilisha taratibu za kuanza ujenzi wa madaraja matano ya Kemishango, Kanoni, Kalebe, Kyanyabasa na Kyetema katika Mkoa wa Kagera.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!