Na Magrethy Katengu– Dar es salaam
Naibu Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano la Tanzania mbaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe Azzan Zungu anatarawa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Mahafali ya 9 Chuo cha Furahika Education College kilicho chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi -VETA yatakayofanyika Agosti 3, 2024 Malapa Jijini Dar es salaam.
Hayo ameyasema Mkuu wa chuo cha Furahika Education College Dkt. David Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 29 2024 ambapo , Amewaalika watu wote hususani wazazi, walezi wageni watakaopelekewa mwaliko i kuhudhuria Mahafali hayo
” Niseme bila kuficha uongozi wa awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kumekuwa na miradi mingi inayounga mkono sekta ya elimu kwa kutoa elimu bure, kikiwemo chuo hicho ambapo Mwanafunzi akichaguliwa kujiunga anakuja na vifaa vyake jambo ambalo limesaidia hata wasio na uwezo kuweza kupata ujuzi hivyo ameomba udhamini kwa mashirika, taasisi au sekta binafsi ili kuunga mkono jitihada hizo kwa kuwezesha vifaa chuoni hapo” amesema Dkt Msuya
Aidha, Chuo bado kinaendelea kupokea wanafunzi hasa wa kozi ya ualimu katika ngazi ya mwaka mmoja, kozi ya social work ngazi ya mwaka mmoja, hotel management ngazi ya mwaka mmoja na miezi sita, masuala ya Bima, mwaka mmoja na miezi sita, mafunzo ya bandari kwa miezi sita na ya mwaka mmoja, ushonaji na nyingine nyingi zinazotoa mafunzo ya Veta” amesema Dkt Msuya
Hata hivyo, Mkuu wa chuo hicho ametangaza Septemba 10 mwaka huu masomo hayo yataanza, hivyo amefafanua namna bora ya kuomba nafasi kwa kuingia kwenye website rasmi ya Furahika ambayo ni www.furahika.or.tz