Home Kitaifa PROF. KITILA AAHIDI BARABARA YA BINTI KAYENGA KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI...

PROF. KITILA AAHIDI BARABARA YA BINTI KAYENGA KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI KUPITIA DMDP

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo akiwa ziarani katika Kata ya Mabibo ameahidi kujengwa kwa kiwango cha Lami barabara ya Binti Kayenga inayounganisha Kata za Mabibo na Manzese.

Prof. Kitila amesema barabara hiyo ni miongoni mwa ahadi zake alizotoa mwaka 2020 kuwa itajengwa kwa kiwango cha Lami na sasa ahadi hiyo inakwenda kutimia.

Amesema barabara hiyo yenye urefu wa KM 1.27 itajengwa kwa gharama ya Sh. Bilioni 2.5 kupitia Mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP).

“Barabara ya Binti Kayenga ni muhimu sana maana inaunganisha mitaa minne na inaunganisha Kata ya Mabibo na Manzese na Rais Dk. Samia ameridhia ijengwe na tayari tenda imeshatangazwa” – Prof. Kitila Mkumbo

“Katika ahadi zangu niliahidi barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami na nchi hii ni kubwa na ina jumla ya Kata zaidi ya 3000 na Mitaa na vijiji zaidi ya 16,000 na vyote vinahitaji fedha hivyo kazi kubwa ya Mbunge ni kupambana kuhakikisha eneo lake linapatiwa fedha, na tumezipata” – Prof. Kitila Mkumbo.

Katika hatua nyingine Prof. Kitila Mkumbo ameahidi kuchangia katika ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kanuni kiasi cha Sh. 500,000 kutoka mfukoni kwake huku akichangia Sh. 5,000,000 kutoka fedha za mfuko wa Jimbo.

Prof. Kitila amesema ofisi hiyo inapaswa kukamilika kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili iweze kutumika ambapo pia amewalipia ahadi ya Sh. 150,000 Viongozi wa CCM Kata ya Mabibo ambao waliahidi kuchangia ujenzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!