PICHA YA PAMOJA : Baadhi ya Washindi wa Vifaa vya Hisense ( TV na Friji ) kampeni ya ZIGO LA EURO CUP na Hisense katika Picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka Tigo , Hisense na PariMatch , muda mchache baada ya kukabidhiwa vifaa vyao walivyoshinda , ikiwa ni hitimisho la Kampeni hii Leo , Julai , 19 , 2024.
Na Adery Masta
Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, imehitimisha kampeni yake ya Zigo la UERO CUP NA HISENSE Kampeni iliyobadilisha maisha ya zaidi ya wateja wao 40 walioibuka na ushindi mbalimbali ambapo wengine wameenda Ujerumani kushuhudia UEFA 2024, wengine wamepata TV na Fridge pamoja na pesa taslimu za Shilingi Milioni Moja Moja.
Washindi wa ZIGO LA EURO CUP NA HISENSE ni wale ambao wanatumia TIGO PESA SUPER APP kufanya miamala, manunuzi na kulipia bili mbalimbali pia wengine ni wale waliokuwa wakibashiri na PariMatch kupitia TIGO PESA SUPER APP.
Akiongea wakati wa kuhitimisha Kampeni hiyo Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutta amewasihi wateja wa Tigo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kutumia mtandao wa Tigo maana kuna mambo mazuri yanakuja muda so mrefu.