Mwenyekiti wa bodi ya Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini nchini FEMATA Yusuph Kazi ameomba Wizara ya TAMISEMI iandae bei elekezi ya tozo kwa maeneo ya wachimbaji wadogo nchini na waisimamie itumike kutoza Wachimbaji wadogo wote nchini ili kuondoa tofauti za tozo kwa wachimbaji wadogo katika Kila Halmashauri nchini.
Amesema hayo wakati akizungumza na Mzawa Online kuhusu maazimio ya mikutano iliyofanyika katika maadhimisho ya Wiki ya Madini mwaka 2024 yaliyofanyika jijini Dodoma hivi karibuni amesema bei hiyo elekezi ipangwe kutumiwa katika Halmashauri zote nchini.
.
Yusuph alisema Wachimbaji wadogo katika Halmashauri zote nchini wanafanya kazi zinazofanana kote lakini wengine wanatozwa tozo ndogo huku wengine wanatozwa tozo kubwa zaidi na kutoa mfano Halmashauri ya Chato ambayo huwatoza Wachimbaji wadogo tozo hadi shilingi milioni 5 kwa mwaka kiasi ambacho kinazidi hata kiasi cha kupata leseni katika Wizara ya Madini ni shilingi milioni 2.
“Tumekuwa tukilalamika huu ni mwaka wa tano pamoja na kukaa vikao kuwaelewesha kwamba tunahitaji kuchimba na tunalipa mapato mengine ya TRA lakini bado wamekuwa wakifunga vitaru vyetu huku wakijua kwamba kwenye Kila uzalishaji tunaozalisha tunalipa asilimia 0.3 Kodi ya service lev inayokwenda serikali kuu na Kodi zingine nyinyi zinazokwenda serikali kuu” alifafanua Yusuph.
“Angalau hizi Halmashauri kupitia Wizara ya TAMISEMI ingeweza kuleta tozo zinazolingana nchi nzima kama ilivyo katika uuzaji wa dhahabu ambayo bei inalingana nchi nzima hivyo na gharama za tozo za maeneo ya uchimbaji, miaro zote zifanane nchi nzima” alisistiza
“Ili tujue kabisa gharama ya kulipa kwaajili ya uwekezaji wa uchimbaji madini ni kiasi fulani ili kuondoa tofauti hizo za tozo kwa wachimbaji wadogo nchini waendelee na uchimbaji bila vikwazo vyovyote wafikie malengo waliyojiwekea ya mwaka 2010/2030 ya maisha ni utajiri na Madini ni utajiri”
ameshukuru na kupongeza serikali kushughulia kero za Wachimbaji wadogo nchini.
Alisema kwasasa Kuna Halmashauri zinatoza tozo ya50,000/-, laki 2/, laki 5, laki 6 na zingine hutoza hadi milioni 5 jambo ambalo hupelekea malalamiko miongoni mwa Wachimbaji wadogo nchini kwani wanaposhindwa kulipa migodi yao hufungwa na kuikosesha mapato serikali pia.
Awali alianza kushukuru kwa jitihada zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili Wachimbaji wadogo nchini ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku ya kuto kuwaondoa Wachimbaji wadogo wenye leseni katika maeneo wanayochimba madini.
Yusuph alitaja kero nyingine iliyoshughulikiwa na serikali ni pamoja na Halmashauri nchini zisitoze tozo kubwa kuliko kiasi kilichopangwa kulingana na Sheria mama.
Pia alishumkuru Rais Dkt Samia kwa kuwezesha vifaa na mitambo kwa Wachimbaji wadogo nchini ambapo Sasa tasnia ya Madini nchini inafanya vizuri na kupongeza kiasi cha kuchangia katika Pato la Taifa ambapo Sasa wanakaribia kuchangia asilimia 10.
“Tunapokea vifaa na mitambo ya aina mbalimbali sambamba na kuongeza bajeti ya Wizara ya Madini tofauti kabisa na miaka mingine” alisema Yusuph