Imeelezwa kuwa asilimia kubwa ya wanaume katika maeneo mbalimbali Nchini hawana nafasi ya uongozi kwenye familia zao kwani nafasi hiyo imeshikiliwa na wanawake kwakuwa wengi wao ndio wameshikilia uchumi wa familia.
Akizungumza na baadhi ya wanaume kwenye semina ya wanaume iliyofanyika wilayani Same Askofu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KkKT Dayosisi ya Same Askofu Charles Mjema amesema akina Baba wengi hawana nafasi tena ya kuziongoza familia zao kwani wenye walioshikilia uchumi wa familia ni wanawake hivyo hao ndio wana mamlaka ya kuzisemea kaya zao.
Askofu Mjema amesema sauti ya mwanaume kwenye familia kwasasa haipo na baadhi ya wanaume wanapotaka kufanya jambo kwenye familia zao nilazima wapate idhini Kutoka kwa wake zao kanakwamba sasa ndio viongozi wa familia.
“Nimezunguka maeneo mbalimbali Nchini nimeona wanaomiliki sehemu kubwa ya uchumi wa kaya ni wanawake na hata kwenye taasisi za fedha wakopaji walio wengi ni wanawake kwanini wao ndio wajasiriamali wakubwa unapotipa kwenye maeneo ya barabara kuu Kutoka Moshi kuelekea Dar es salaam wafanyabiashara waliopo njiani wengi ni wanawake”
“Alisema Askofu mjema”
Mjema amesema wanaume waliowengi wamejisahau katika kutekeleza na kusimamia vyema nafasi zao kitu ambacho sasa kimewafanya wao kukosa nafasi ya kuwa viongozi wa familia huku akiwahimiza wanaume kurudi kwenye nafasi zao na kuendelea kuwa viongozi katika familia ilikusimamia maadili na makuzi ya mtoto.