Home Kitaifa HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAONGEZA NGUVU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA...

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA YAONGEZA NGUVU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KIMKAKATI

Halmashauri ya Jiji la Tanga imesema kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 inatarajia kuongeza nguvu za Utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati ya Jiji ikiwamo Ujenzi wa Masoko,uwekaji wa Taa za Barabarani pamoja, maeneo ya Mapumziko na Kuongeza vyanzo vya Mapato ili kuendelea kuongeza Ukusanyaji wa Mapato Nchini.

Akizungumza Jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya nne,Mchumi wa Halmashauri hiyo Simeon Mzee,alisema Halmashauri ya Jiji la Tanga imeshuka nafasi ya kwanza kwa Ukusanyaji wa Mapato,hivyo itaongeza nguvu kwenye uboreshaji wa Huduma za kijamii ili Wananchi wa Jiji hilo wapate fursa ya kuona Matunda ya Kodi zao,

Hivi karibuni Halmashauri yetu imeshika nafasi ya kwanza katika Majiji yote hapa Nchini, hivyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Halmashauri yetu kutekeleza Miradi yote ya Kimkakati ikiwamo Ujenzi wa Masoko likiwamo Soko la Mlango wa Chuma,tunatarajia kuweka Taa za Barabarani zaidi ya 100 kwenye kata hususani zilizopo Katikati ya Jiji,Ujenzi wa maeneo ya Mapumzik(Forodhani)ambapo tayari Mkandarasi ameshaanza pamoja na Miradi mingine ya Vituo vya Afya na Elimu“alisisitiza Mzee

Akichangia hoja za Mchumi,Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu alisema kunahitajika mikakati mizito pamoja na kupitia mapungufu kwenye Sekta ya Elimu ambapo inaonekana Matokeo ya Sekondari haifanyi vizuri kila mwaka ukilinganisha na Matokeo ya Msingi,

Matokeo ya Sekondari hayaridhishi kila mwaka,hivyo Ofisa Elimu ni lazima tufanye Uchambuzi ni kwanini tumeshuka,lakini pia tunatakiwa tuhakikishe tunakuwa na miundombinu yote Shuleni,nilazima tufanye Uchambuzi wa kwanini tumeshuka kwenye asilimia“alisema Ummy

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Abdalrhaman Shilow aliwapa mikakati mizito Watumishi wa Halmashauri hiyo hususani wakuu wa Idara kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi zaidi na kuweka kipaumbele Maslahi ya Wananchi.

Tumeshika nafasi ya kwanza kwenye ukusanyaji wa Mapato sawa lakini Nini kinafuata Baada ya kuongoza? Alihoji,

Nilazima tuhakikishe Huduma za Kijamii zinavadilika ili ziendane na kiwango Cha mapato ambayo Wananchi ndio wanaotoa,hivyo ni nilazima zionekane kwa vitendo,Huduma za Kijamii ziwe nzuri ili Wananchi wafurahie Mapato Serikali yao alisisitiza Shilow

Aliwataka wakuu wa Idara kufanya kazi kwa weledi zaidi na kujiepusha na vitendo viovu na kufanya kazi kwa Mazoea,

Msifanye kazi kwa Mazoea,tunataka tupande zaidi ya hapa tulipo, hivyo tunawapongeza wakuu wa Idara na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ndugu yetu Spora Liana,kwa kutuletea heshima kubwa, Jiji letu linang’ara Sasa hivi kuanzia kwenye Usafi,ukusanyaji wa Mapato Hadi kwenye Huduma za Kijamii“alisema Shilow

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!