Home Kitaifa OMBI LATOLEWA KUSAIDIA JAMII HUSUSANI HUDUMA ZA KIAFYA

OMBI LATOLEWA KUSAIDIA JAMII HUSUSANI HUDUMA ZA KIAFYA

Pichani Mwenyekiti wa Jumuiya ya Taasisi ya Khoja Shia Ithnasheri Charitable Eye Centre Mohamed Raza Dewj katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
Pichani Daktari wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Amiri Kanji

Na Magrethy Katengu

Taasisi za kiserikali na zisizo za kiserili zimeombwa kujitokeza kusaidia changamoto zinazoikabili Jamii hususani katika kiafya kwani walio wengi hukabiliwa na changamoto ya kukosa fedha
hali inayopelekea kufika hospitali ugonjwa ukiwa imefikia hatua ya mwisho hivyo kushindikana kutibika.

Ombi hilo limetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Taasisi ya Khoja Shia Ithnasheri Charitable Eye Centre Mohamed Raza Dewj katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo wameweka Kambi ya matibabu ya macho bure na magonjwa mengine yasiyo ya yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari presha na kutoa dawa pamoja na upasuaji jicho kama limegundulika lina tatizo.

Leo tunaadhimisha siku ya kuuwawa kwa mjukuu wa Mtume (saw)Imamu Hussein miaka 1300 iliyopita ,Imamu huyu wakati anapigania dini alipigwa na kuuwawa na damu yake ikamwagika na ndio maana tupo hapa kwa kuchangisha damu na kuwapatia matibabu wagonjwa bure ikiwa ni ishara ya kumuenzi“amesema Dewji.

Hata hivyo amesema walianza kutoa huduma hiyo Agosti 25 mwaka huu na zaidi ya wagonjwa mia nane hadi Jana wamejitokeza zaidi ya wagonjwa mianane kupatiwa huduma huku wengine wakigundulika na mtoto wa jicho hivyo tutawafanyia upasuaji bure kwa kuwapangia tarehe ya kufika hospitali yetu ya Temeke kupatiwa huduma hiyo.

Kwa upande wake Daktari wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Amiri Kanji amesema zaidi ya wagonjwa mia saba wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kati ya hao tumewagundua walio wengi Wana matatizo ya kisukari presha na wengine wanaokutwa na magonjwa hayo wamebainika hawana dalili yeyote .

Tunawapima wanaokuja kupima huwa wamefika hatua ya kuona kuwa hawezi kukojoa hivyo tunawapatia ushauri nasaha na kuwapatia matibabu bila kuwabagua dini,rangi,kabila kwani sisi wote tumeumbwa na Mungu si budi kubaguana“amesema Amiri

Naye miongoni mwa waliojotokeza kupima macho Yakobo Majombe Mkazi wa Kibaha amesema yeye amekuja kwa mara ya kwanza huduma zao ni nzuri kwani nilikuwa nasumbiliwa na macho kuuma na kuwasha hivyo anawasihi wengine kujitokeza wasikae nyumbani.

Kwa upande wake Farida Salehe amesema wanavipimo vizuri sana kwani yeye amepimwa macho na presha pamoja na kisukari hivyo watu wasidanganyane waende wakatibiwa Ili kusaidia wasiende wakiwa wamefikia hatua ya mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!