Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amewatoa hofu wakazi wa wilaya hiyo ambao hawajahesabiwa hadi sasa kuwa watahesabiwa ndani ya muda uliosalia.
Kauli hiyo ya Jokate imekuja kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya wakazi kuwa hawajahesabiwa hadi sasa.
Akizungumza na Mwananchi Jokate amesema kazi hiyo itafanyika kama ilivyopangwa na tayari makarani wameongezwa katika maeneo ambayo hayajafikiwa.
“Hakuna ambaye hatahesabiwa wote watafikiwa, kuna makarani ambao tayari wamemaliza kuhesabu katika maeneo waliyopangiwa hawa tayari tumeshawaongezea maeneo mengine.
“Hili limeanza kwa makarani waliokuwa kata ya Miburani kule wameshamaliza kazi hivyo wanaamishiwa Chamazi kule kuna uhitaji mkubwa na lengo la hili ni kuhakikisha watu wote wanafikiwa,”.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ofisi ya taifa ya Takwimu (NBS) Amina Msengwa amesema utaratibu huo umeanza katika maeneo ambayo makarani wamemaliza kazi.
“Kwenye mfumo kila karani anaonekana eneo lake kama amemaliza tunawakusanya kwa pamoja mfano hawa wa Miburani tumechukua 45 wanaenda Chamazi,”amesem Amina.