Home Kitaifa WATUMISHI 10 WA HALMASHAURI YA SENGEREMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UBADHIRIFU WA FEDHA...

WATUMISHI 10 WA HALMASHAURI YA SENGEREMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA MAPATO

Juni 3, 2024 Watumishi 10 wa nafasi na kada mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerama wamefikishwa Mahakamani kwa Makosa ya Matumizi mabaya ya madaraka pamoja na Ufujaji na Ubadhilifu wa Sh. Millioni 87 kinyume na vifungu vya 31na 28 vya PCCA sura ya 329 na marejeo yake ya mwaka 2022.

Washtakiwa hao katika nyakati tofauti Kati ya Julai 01/2016 hadi Februari 15,2021 wametenda makosa hayo wakiwa na nia ovu, walitumia madaraka yao vibaya na kushindwa kuwasilisha fedha za mapato ya Serikali zaidi ya Sh. Millioni 87 kwenye akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Mapato hayo ni makusanyo mbalimbali fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.

Kitendo cha kutokuwasilisha Benki fedha hiyo ya Serikali ni kinyume na kifungu cha 50(5) ya Memoranda ya Fedha za Halmashauri za Mwaka 2009, ambazo kimsingi walijipatia manufaa binafsi.

Mashauri 10 dhidi ya watumishi hawa wa Serikali yamefunguliwa Juni 3,2024 mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi Mhe. Evod Eugen Kisoka, na yamesomwa Mahakamani hapo na Waendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Wakili Moses Malewo, Saida Salum na Maxmillian Kyabona.

Baadhi ya Watumishi waliofikishwa Mahakamani ni:-

  1. Revocatus Reuben Kasana mwenye shauri namba 14931/2024
  2. Francisca Mathew Temu mwenye case namba 14927/2024
  3. Elias Amos Magulu mwenye case namba 14942/2024
  4. Kalambizi Leonard Gervase mwenye case namba 14924/2024
  5. Benedict Kanfune Phillip mwenye case namba 14922/2024
  6. Faida Revocatus Majaliwa mwenye case namba 14932/2024
  7. Emmanuel Magida Mwitagula mwenye case namba 14920/2024
  8. Felix Chacha Boniphace mwenye case namba 14921/2024
  9. Jenipher Maige Mashamba mwenye case namba 1433/2024 na
  10. lluminata Samwel Suleiman* mwenye case namba 14930/2024.

Washtakiwa wote wamekana makosa yao na wapo nje kwa dhamana.

Kesi hizo zitakuja tena Mahakamani Juni 19 na 26, 2024 kwa ajili ya Hoja za Awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!