Na Boniface Gideon -ARUSHA
Kampuni ya huduma za Utalii kupitia Hotel ya Johari Rotana Dar es Salaam imewataka Watanzania kutenga muda wa kufanya Utalii ili kuimarisha Mahusiano ya familia na kupunguza migogoro ya ndoa.
Johari Rotana Dar es Salaam yenye makao makuu jijini Dar es Salaam inasimamia hotel za kitalii zenye hadhi ya nyota tano imeshiriki maonyesho ya Utalii Mkoa wa Arusha maarufu kama ‘KILIFAIR 2024’ yaliyomalizika jana.
Akizungumza wakati wa kufunga maonyesho hayo, Afisa Msaidizi wa Mauzo kutoka Johari Rotana Dar es Salaam Rukia Chuma amesema ni vyema Watanzania wakajiwekea utaratibu wa kufanya Utalii wa ndani,
“kufanya Utalii sio kwa ndugu zetu wa nje tu, hapana bali ni kwa watu wote na kufanya Utalii sio lazima uwe na pesa nyingi, unaweza kwa matumizi yetu ya kila siku unaweza ukajiwekea utaratibu wa kuweka akiba kidogo kidogo, halafu ukaangalia ni muda gani muafaka wa kutoka na familia yako kama ni majira ya sikukuu za mwisho wa mwaka ama maadhimisho fulani kama vile siku ya wapendanao, siku ya Wanawake au wakati ambao hauna sikukuu wala maadhimisho yoyote” Alisisitiza Rukia
Alisema utaratibu wa kufanya Utalii una faida nyingi kwa maisha ya kila siku ikiwemo kuimarisha Mahusiano ya familia na kuondoa msongo wa mawazo.
“kufanya Utalii una faida nyingi kwa maisha ya kila siku unaondoa migogoro ya familia na kuimarisha Mahusiano ya familia, Utalii unasaidia kuondoa msongo wa mawazo na kuimarisha Afya ya akili, mfano ukija hotelini kwetu utapata fursa ya kufurahia vitu vingi, maana tuna kila aina ya huduma kuanzia ndoa hadi familia kwa hiyo utafurahia maisha na utaondoa msongo wa mawazo kabisa” Alisema Rukia
Aliongeza kuwa gharama za huduma za Hotel Johari Rotana Dar es Salaam ni za gharama nafuu.
“Gharama zetu ni nafuu sana, kila mtu anazimudu,tunatoa huduma kuanzia harusi, ambapo mke na mume au kikundi kinaweza kuja kufanya shughuli zao, tuna huduma za vyakula vya Mataifa mbalimbali ikiwemo China ambayo ndio soko kuu kwa sasa, kwa hiyo niwakaribishe Watanzania na wasio Watanzania waje wafanye Utalii kwetu na watafurahia Utalii wetu” Aliongeza Rukia