Mbunge wa Jimbo la kinondoni Mhe. Tarimba Gulam Abbas ametoa kadi za bima kwa wenyeviti wa mashina zitakazoweza kuwasaidia katika matibabu hadi pale atakapoachia ubunge wa jimbo hilo.
Amesema hayo katika kikao kilichofanyika mwananyamala wilaya ya kinondoni ambapo amewataka wenyeviti hao kuweza kusimamia vyema zoezi la sensa ili kutoa takwimu ambazo ni sahihi zitakazosaidia serikali kitekeleza vyema ilani ya chama cha mapinduzi.
Ameongeza kwa kusema kuwa serikali imekuja na mipango ya maendeleo ambayo inategemea umuhimu wa takwimu ili kujua idadi ya watoto watakaoweza kujiunga na shule ya awali,elimu ya sekondari,elimu ya vyuo vikuu pamoja na utatuzi wa ukosefu wa ajira kwa vijana.
Hata hivyo upatikanaji wa takwimu sahihi utaweza kirahisisha uundaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na matokeo ya upatikanaji wa sensa.