Home Kitaifa EXOTIC TOURS & SAFARIS WATANGAZA NEEMA.ONGEZEKO VIVUTIO VYA UTALII ZANZIBAR.

EXOTIC TOURS & SAFARIS WATANGAZA NEEMA.ONGEZEKO VIVUTIO VYA UTALII ZANZIBAR.

Meneja Masoko na Mauzo kutoka kampuni ya huduma za Utalii Visiwani Zanzibar ya Exotic tour’s & Safari’s Fatma Muhiddin, akizungumza na Waandishi wa Habari jana wakati wa kufunga maonyesho ya Utalii Mkoa wa Arusha maarufu kama ‘KILIFAIR’

Na Boniface Gideon – ARUSHA

Kampuni ya huduma za Utalii Nchini ya Exotic Tours & Safaris imetangaza neema zakuongezeka kwa vivutio vya Utalii Visiwani Zanzibar, ikiwemo Utalii wa Bahari , kuzama kwa jua na nyengine, kwa watalii wa ndani na nje ya Nchi ambao watatembelea vivutio vya Utalii Visiwani na Bara.

Aidha kampuni hiyo imewashukuru makampuni yote yanayotoa huduma za Utalii hapa Nchini na nje kwa ushirikiano wao, nakwamba wataendelea kunufaika kwa fursa za Utalii kupitia wageni wanaotembelea Visiwani Zanzibar na hawatosita kutoa ushirikiano.

Meneja Mauzo na Masoko Fatma Muhiddin ,amewaeleza Waandishi wa Habari kwenye maonyesho ya Utalii Mkoa wa Arusha maarufu kama ‘KILIFAIR‘ ,kuwa kwasasa huduma za Utalii Nchini zinaendelea kuimarika baada ya mtikisiko wa ugonjwa wa COV-19 hivyo watalii wa ndani na nje ya Nchi kutembelea vivutio mbalimbali Visiwani Zanzibar na Bara,

Kampuni yetu ni kongwe kwa miaka zaidi ya 20 kwenye Sekta za Utalii Nchini, inamilikiwa na Mzawa, tunatoa huduma zote za Utalii,niwaombe Watanzania tuupende Utalii wetu,njooni mjionee uzuri wa nchi yetu,Kuna Bahari nzuri na fukwe zake,Kuna hifadhi na mbuga nzuri za wanyama,kuna view point na jua kuchomoza na kuzama,bila kusahau makumbusho ya Taifa” Amesema Fatma

Fatma amesema wataendelea kutoa fursa nyingi za ajira kwa Vijana wenye sifa katika Sekta za Utalii Nchini,“tutaendelea kutoa fursa kwa Vijana wote wenye sifa,sio lazima sisi tuwapatie ajira,bali tunauwezo wa kumuunganisha kijana na kampuni nyengine za Utalii, niwaombe Vijana wenzangu tuchangamkie fursa za kusomea masuala ya Utalii ili uwe na sifa” Amesisitiza Fatma

Kwaupande wake Fathiya Ayoub ameyashukuru makampuni yote Utalii Bara na Visiwani kwaushirikiano mkubwa katika kukuza Sekta ya Utalii pamoja na Serikali kwakuweka mazingira mazuri na wezeshi hali inayofanya Sekta ya Utalii kuzidi kukua Nchini,

Tunaishukuru sana Serikali kwakutuwekea mazingira mazuri na wezeshi, lakini pia tunayashukuru makampuni yote yanayotoa huduma za Utalii Nchini,tumekuwa na Furaha sana kufanya nao kazi,niwakaribishe Watanzania kutembelea vivutio mbalimbali Visiwani Zanzibar na Bara na sisi tutaendelea kushirikiana kwakutoa huduma nzuri” Amesema Fathiya

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!