Home Kitaifa MCHUNGAJI MWAMPOSA ‘BULLDOZER’ AWEKA WAZI KUHUSU SENSA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUHESABIWA

MCHUNGAJI MWAMPOSA ‘BULLDOZER’ AWEKA WAZI KUHUSU SENSA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUHESABIWA

Mchungaji na Nabii wa kanisa la Arise and Shine nchini Tanzania Apostle Boniface Mwamposa Bulldozer ameweka bayana utayari wake katika zoezi la kuhesabiwa kupitia Sensa Agosti 23 mwaka huu.

Mwamposa ambae amekuwa kiongozi mahiri wa imani ya kikristo nchini hata kujizolea umaarufu mkubwa kama “Bulldozer” ameeleza namna zoezi la sensa lilikua likifanyika hata zamani katika vitabu vitakatifu vinajieleza na kuwaasa watanzania kutopotoshwa juu ya zoezi la kuhesabiwa nchini.

“Sensa ni jambo la baraka kiimani, wakati Yesu anazaliwa ilitangazwa amri na Kaisari kuwa watu wote wahesabiwe, hata Yesu alipozaliwa alizaliwa katika holi la ng’ombe sababu nyumba za wageni zilijaa watu waliokuwa wamerudi kwao kuhesabiwa.”

Mchungaji Mwamposa amewaasa watanzania kujitokeza kuhesabiwa na kufurahia jambo hilo kwani linaleta baraka kwa wananchi na nchi kiujumla.

“Furahia kuhesabiwa ili ujulikane kama mmoja wa watanzania walio mchini, mimi niko tayari kuhesabiwa na wewe ukahesabiwe.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!