Home Kitaifa NSSF YAJIPANGA KUWAFIKIA SEKTA ISIYORASMI KIKAMILIFU

NSSF YAJIPANGA KUWAFIKIA SEKTA ISIYORASMI KIKAMILIFU

Na Emmanuel Kawau

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii NSSF umewataka wafanyakazi wa sekta binafsi na wale wasio na sekta rasmi kujiunga na mfuko huo kwaajili kwa hiyari na kuwa na kinga madhubuti pale wanaposhindwa kufanyakazi kwa namna yoyote.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mkuu wa NSSF Masha Mshomba wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya mfuko huo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2021/2022 na mwelekeo wa vipaumbele vya bajeti 2022/2023 ambapo amesema mifuko ya hifadhi ya jamii inakinga maisha yako ya sasa na baadae.

Katika Dunia nzima hakuna kinga madhubuti na ya uhakika katika maisha yako ambayo unaweza kujiwekea kama kuchangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii, ni kinga hasa inayolenga kukuhudumia pale unapopata majanga mbalimbali Binadamu tumeumbwa hata kama Mwenyezi Mungu atakuweka sana lakini unakuwq mzee na uwezo wa kufanyakazi unapungu” Alisema Mshombo.

NSSF katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 inampango wa kuteleza maboresho ya mkakati wa uchangiaji wa hiyari kutoka kwa sekta isiyorasmi maboresho hayo yatasaidia kupunguza changamoto zilizopo na kuvutia watu wengi zaidi ukizingatia sekta hiyo ndiyo yenye watu wengi zaidi.

Kitu kizuri zaidi ni kuhakikisha tunatoa mafao ambayo yanavutia zaidi kwa sekta isiyorasimi,sekta hii inawatu wengi wakiwemo , bodaboda,wakulima na wavuvi

Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha mfuko umejipanga kuongeza wanachama pamoja kudhibiti mifumo ya ukusanyaji michango kwa kuboresha tahama ya mifumo hiyo.

Aidha amesema NSSF katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 wamejipangia kukusanya Trion 1.62 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 14% ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo walijipangia kukusanya Trion 1.38 pia wanatarajia kukusanya mapato yatokanayo na uwekezaji katika miradi mbalimbali yapatayo Tzs Bilioni 691.

Tunatarajia katika mwaka huu wa fedha uwekezaji wetu ukue na kufikia Trioni 6.1 sawa ongezeko la asilimia 17% ukilinganisha na uwekezaji uliopo kwa sasa wa Trioni 5.2,ukiangia mfuko wetu unakua na si tu kwa maneno bali na kwa vitendo na ni jambo la kuvutia sana kwa wanachama wetu kuona mfuko wao unakuwa endelevu” alisema Masha.

Katika sehemu ya vipaumbele vyetu ni kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato na matumizi lengo ni kuhakikisha fedha za wanachama zinakuwa salama na kusaidia mfuko kuwa himilivu.

Pia NSSF inatarajia kulipa mafao kwa wanachama wake yenye thamani ya Shilingi bilioni 828.91 sawa na ongezeko la asilimia 26 ukilinganisha na mwaka uliopita ambayo walilipa Shilingi Bilioni 659.76

NSSF tumejiwekea mikakati ya kuhakikisha tunalipa mafao kwa muda uliowekwa kisheria ambapo ni ndani ya siku sitini baada ya mwanachama kutimiza vigezo vya kujitoa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!