Home Kitaifa MAMA TUNU PINDA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA AMANI NCHINI –...

MAMA TUNU PINDA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA AMANI NCHINI – UPF

Na Scolastica Msewa, Dar es Salaam
Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda ameteuliea kuwa Mwenyekiti wa shirikisho la amani duniani UPF Kanda ya Tanzania (Universal Peace federation- UPF) kwa miaka miwili baada ya kukabidhiwa na Balozi wa shirikisho la amani duniani bara la Afrika UPF Adama Doumbia lengo la Uenyekiti huo ni kuhamasisha amani miongoni mwa watanzania bila kubagua dini, Madhehebu, mila, Viongozi wa Chama na serikali, Wabunge na wananchi kuanzia ngazi ya mtu mmoja, familia hadi taifa.

Makabidhiano hayo yanefanyika kwenye hafla fupi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya na Mashirikisho ya Amani ya dini, madhehebu mbalimbali nchini na Viongozi wa kimila.

Akimkabidhi barua ya utambulisho wa nafasi hiyo ya Uenyekiti Balozi wa shirikisho la amani duniani bara la Afrika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Amani duniani Kanda ya Afrika UPF kutoka nchi ya Ivory coast Adama Doumbia amesema UPF ni Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO) ambayo kazi yake kubwa ni kutangaza na kusimamia amani baina ya watu wa dini zote na makabila yote na nyanja zote ambalo Makao makuu yake ni nchini Korea.

Aidha Adama ameagiza kuandaliwa kwa sherehe kubwa maalumu ya kumtambulisha Mwenyekiti kiti huyo mpya wa Shirikisho hilo la Amani nchini Tanzania ambaye atakabidhiwa rasmi na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mama Marie Kigalu ambapo Viongozi mbalimbali watahudhuria.

Aidha Mama Tunu Pinda alishukuru kwa uteuzi huo na kuahidi kuendeleza ushirikiano kwa taifa, bara la Afrika na duniani nzima harakati za kulinda amani sawa na malengo ya taasisi hiyo ya UPF.

Amesema Tanzania ni nchi inayosifika kwa amani na utulivu hivyo ameahidi kuendeleza kulinda sifa hiyo ya taifa letu kwa kutoa elimu katika makundi yote hasa kwa kutumia kundi la tasinia ya Habari na Waandishi wa Habari.

Kiongozi wa kitaifa wa Shirikisho la Amani duniani Kanda ya Tanzania Dr. Stylos Simbamwene amesema suala la amani huanzia na mtu mmoja, familia, Jumuiya mbalimbali, taifa na duniani kwa ujumla.

Amesema kilichofanyika leo ni hafla ya kushuhudia kubadilishana kwa kukabidhiana Uongozi kwa Viongozi waliokuwepo na Viongozi wapya ambapo Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo nchini aliyeteuliwa ni Profesa Beneza Mwang’ombe.

Wengine walipewa Ubalozi wa Shirikisho hilo la Amani duniani katika mikoa mbalimbali nchini kuwa ni pamoja na Dkt. Angella Gloria Bondo, Dr. Bruno Mwakiborwa, Dr.Amos Lwitiko Mwakabana, Dr. Chelestino Simbalimile Mofuga, Archbishop, Aliyekuwa Sheikhe wa mkoa wa Dar es salaam Dr. Alhad Mussa Salum na Julius Lissu Nyenje.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!