Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 18, 2024 amezungumza na wakazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassam anaguswa na maisha ya Watanzania na anataka kuona watanzania wanahudumiwa.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewaeleza wakazi hao kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia ipo imara na inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuangalia mahitaji ya kila eneo nchini na kuyafanyia kazi