Home Michezo MWADUI WAHAMIA KOROGWE, YAWEKA MIKAKATI KUPANDA LIGI KUU.

MWADUI WAHAMIA KOROGWE, YAWEKA MIKAKATI KUPANDA LIGI KUU.

Na Boniface Gideon, TANGA

Timu ya Mwadui ya mkoani Shinyanga ambayo ilitamba miaka kadhaa kwenye Ligi kuu Tanzania Bara sasa ni Rasmi imenunuliwa na Mfanyabiashara maarufu wa Madini Wilayani Korogwe mkoani Tanga na Mkoa wa Shinyanga Ahmed Waziri Gao na sasa ni Rasmi makao yake makuu yatakuwa mkoani Tanga.

Ikumbukwe kuwa Mwadui kwasasa imetinga hatua ya Nusu fainali ya ligi Daraja la pili maarufu kama First League na endapo itafanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali ya ligi hiyo basi itakuwa imejihakikishia kupanda ligi Daraja la Kwanza maarufu kama ‘Championship’ kwa msimu ujao.

Mkurugenzi wa Timu hiyo Ahmed Waziri Gao amewaeleza Waandishi wa Habari Kuwa ,Timu hiyo kwasasa imenunuliwa kutoka kwa wamiliki wa awali na sasa ni Rasmi imehamia wilayani Korogwe,

“Tumeamua kuweka nguvu kubwa ya fedha ili tuipandishe timu yetu Ligi kuu,hivyo wadau wa soka hasa mkoani Tanga nawaomba waisapoti timu yao ” Amesema Gao

Kuhusu kubadilisha jina la Timu hiy,Gao amesema wapo kwenye mchakato kama wataweza kubadilisha jina lakini wanaangalia jina ambalo litaendana na mila na Desturi za Korogwe na Mkoa wa Tanga,
“Unajua mimi ni mzaliwa wa Korogwe mkoani Tanga,hivyo huwa nikiwa huko ninatabia za kuomba timu ili niwekeze lakini sasa hivi nimeinunua timu hii moja kwa moja tunaangalia jina ambalo litaendana na mila na Desturi za asili yetu, Korogwe kuna Mdumange lazima tuangalie asili hiyo”
amesema Gao

Kwa upande wake Kocha wa Timu hiyo, Salhina Mjengwa amesema wamejipanga kupanda ligi kuu hivyo nilazima watwae Mataji yote wanayoshiriki ikiwemo First league.

tumejipanga kupanda ligi kuu na tutahakikisha tunatwaa Mataji yote tunayoshiriki ili tupate fursa yakupanda Ligi kuu, maandalizi ya kuelekea hatua ya nusu fainali yamekamilika na tupo tayari kwa michezo ya hatua inayofuata” Amesema Mjengwa

                   Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!