Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Elirehema Joshua Doriye kuwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
Aidha Dkt. Doriye aliwahi kuwa Mkurugernzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Vilevile Dkt. Samia memteua Bw. Christopher Derek Kadio kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo anachukua nafasi ya Bi. Esther Hellen Lugwisha ambaye amemaliza muda wake.
Hayo yameelezwa kwenye taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus leo Mei 06, 2024 jijini Dar es Salaam.