Home Kitaifa SHEKH WALID AONGOZA WANANCHI DAR KUFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

SHEKH WALID AONGOZA WANANCHI DAR KUFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI

Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limeungana na Watanzania wengine nchini kushiriki katika dua ya kuwaombea ikiwemo kuwatembelea na kugawa misaada mbalimbali Waathirika wa mafuriko wilayani Rufiji ikiwa ni sehemu ya kurejesha faraja kwa wananchi hao kufuatia changamoto iliyowakuta.

Shekhe Mkuu wa BAKWATA mkoa wa Dar es salaam Sheikh Walid Alhad Omary amesema uamuzi wa kutembelea wilayani Rufiji unaonesha kutii mafundisho ya mtume MUHAMMAD S.W ya kuwahurumia watu wenye matatizo.

Sheikh Walid ameongeza misaada hiyo iliyotolewa kwa ushirikiano wa wananchi wa Dar es salaam kutoka madhehebu mbalimbali ni ishara ya kumuunga mkono Rais Dkt. SAMIA Suluhu Hassan pamoja na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi.

“Tulipotangaza kuleta msaada kwa ndugu zetu wa walioathirika na mafuriko ya Mto Rufiji huko Wilayani Kibiti na Rufiji mkoani Pwani watu mbalimbali wa Dini na madhehebu mbalimbali walijitojeza kutoa misaada yao hivyo misaada hii ni ya Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam sio wa Dini ya kiislamu” alisema Sheikh Walid wakati alikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele.

Sheikh Walid allmewataka Watanzania kuiombea nchi yetu ili mvua zinazoendelea kunyesha nchini ziwe za baraka sio zinazoleta athari kwa jamii nchini ikiwemo Wananchi wa Wilaya za Kibiti na Rufiji.

Aidha Sheikh huyo alikabidhi misaada hiyo ikiwa katika magari matatu aina ya fuso yakiwa na Sukari, unga, mchele, vyandarua, maharage, mafuta ya kupikia, nguo za watoto, nguo za wakubwa, pampas za watoto, mashuka, kanga na sabuni nakusema kwamba bado wanaendelea kuchangia Waathirika hao.,

Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amemshukuru sheikh Walid na Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliochangia msaada huo na kumuomba aendelee kuwaombea wananchi wa Rufiji wanaopitia katika mazingira magumu kwani athari za mafuriko hayo ni kubwa katika Wilaya hiyo.

Aliomba Wadau mbalimbali msaada wa mafuta kwaajili ya kuwezesha magari kwa usambazaji wa vyakula na huduma kwa waathirika wa mafuriko hayo hasa kutokana na miundombinu kuharibika kutokana na mafuriko nakusababisha magari madogo kutopitika baadhi ya maeneo.

Taasisi nyingine zilizoambata na Sheikh Walid ni pamoja na uongozi wa jumuiya ya jumuiya ya Rahma Foundation na Jumuiya ya IDDEF ya nchini Uturuki ambao nao walikabidhi misaada yao ya vyakula na mafuta ya kupikia ambayo waliweka kwenye mfuko maalumu na kukabidhi wao wenyewe kwa waathirika hao katika Kambi ya Chumbi B wilayani Rufiji.

Mwenyekiti wa juiya ya Rahma Foundation Abdul Hameed Hussein Khan alisema wamekuja kutoa msaada huo ilikutoa faraja kwa waathirika hao wa mafuriko wilayani Rufiji.

Na Scolastica Msewa, Rufiji

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!