Home Kitaifa MWENYEKITI WAZAZI WA CCM TAIFA AKABIDHI MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI...

MWENYEKITI WAZAZI WA CCM TAIFA AKABIDHI MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI NA KIBITI

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni mfariji Mkuu nchini amekuwa wa kwanza kutoa misaada ya faraja kwa waathirika wa matukio mbalimbali nchini ikiwemo waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji kwa Wilaya za Kibiti na Rufiji mkoani Pwani kwa kupeleka tani zaidi ya 300 za chakula yeye binafsi na kusimamia usalama na huduma bora zinapatikana kwenye kambi zote za waathirika wa Mafuriko na majanga mengine yaliyotokea nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa jumuhia ya Wazazi wa CCM taifa Fadhil Rajabu Maganya akiwa katika Kambi ya Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji huko Chumbi B wakati alipokuwa kwenye Ziara ya siku Moja kujionea athari za mafuriko hayo na kupeleka misaada ya vyakula, mavazi na magodoro kwa waathirika hao.

Maganya alisema Rais Dkt Samia ndiye anaguswa na maisha ya Watanzania na kama ambavyo amekuwa siku zote mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Watanzania wanakuwa salama na wanafarajika.

“Yeye alikuwa wa kwanza binafsi bila serikali akaleta tani 300 ambazo ni tani 100 za maharage, tani 100 za unga na tani 100 za mchele ili nyinyi Wananchi muweze kujikimu na kuondokana adha mliyokuwa mnaipata ya njaa kutokana na mafuriko hayo”

Alisema serikali imetenga maeneo kwaajili ya Waathirika hao wa mafuriko ya Mto Rufiji ili wahame kabisa mabondeni na maeneo hatarishi ya Mto huo ili wasogee maeneo salama hivyo amewataka kukubali agizo hilo.

“Lipokeeni hili jambo hameni huko hamieni maeneo ambayo ni salama maana mvua hizi pengine Sasa tumezipokea kama zilivyo hatujui kesho, mwaka au baada ya miaka mitatu au minne ijayo mvua zitakuwa je na zitakuja kwa namna gani hivyo tuwaombe kwamba kama kadri serikali inavyoshauri tuisikilize serikali tuzingatie ushauri wao” alisema.

“Endeleeni kuwa wasikivu maana hakuna ambaye angependa Wananchi wake wapate athari kama hizi lakini serikali ya CCM kupitia Mheshimiwa Rais na wawakirishi wake kuanzia ngazi ya mkoa na Wilaya” alisema Maganya.

Aidha aliwataka Watanzania kupuuzia upotoshaji wa taarifa za Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Julias Kambarage Nyerere unaofanywa na baadhi ya watu ambapo ukweli ni kwamba Mafuriko katika Wilaya hizo yamekuwa yakitokea kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Katika Ziara hiyo pia Mwenyekiti huyo alikabidhi misaada mbalimbali ya kukidhi mahitaji ya Waathirika hao ikiwa ni pamoja na magodoro 30, sabuni za unga viloba 19, vyandarua balontano, mablanketi mabalo mbili, nguo za watoto, akinamama na nguo za wanaume, sahani 240, ndala dazani mbili, mikate 500, kilo 750 za sukari, unga viloba 200,

Mjumbe Baraza Kuu WAZAZI Taifa (Viti 3- Tanzania Bara) Ally MANDAI alisema tayari serikali imetenga zaidi ya bilioni 66 kwaajili ya kufanyia ukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na maji ya mvua yanarudishwa kwa haraka.

Mwenyekiti wa jumuhia ya Wazazi wa CCM mkoa wa Pwani Jackson Kituka alimuahakikishia Mwenyekiti huyo wa jumuhia ya Wazazi wa CCM taifa kwamba CCM itashinda kwa kishindo katika vijiji na vitongoji vyote mkoa wa Pwani.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema katika Wilaya za Kibiti na Rufiji Kuna kambi nne za Waathirika wa mafuriko ambapo Moja ipo Rufiji na kambi tatu zipo Wilaya ya Kibiti ambako Wananchi wamestriwa na serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!