Na Theophilida Felician, Kagera
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa Kagera kupitia kwa meneja wake Castro John ametoa wito kwa wafanyabiashara Kagera wanaositahili kulipa kodi kufanya hivyo kama yalivyomakusudi ya serikali.
John meyaeleza hayo hii leo Tarehe 25 Aprili 2024 kwenye kikao na waandishi wa habari kilichofanyika makao makuu ya TRA Kagera yaliyopo Manispaa ya Bukoba.
Amesema kwamba ulipaji kodi ni wajibu wakila mfanya biashara ili kusaidia mapato ya serikali iweze kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
Amefafanua kuwa kuna vitu muhimu kwa mfanyabiashara anapaswa kivizingatia katika uendeshaji wa biashara hususani utoaji wa risti za EFD kwa wanunuzi wa bidhaa.
“Tunahakikisha kila mtu tunatarifa zake za mwenendo wa utoaji risiti hizo, hiyo ikiwa ni moja ya njia yakutusaidia kuwabaini wale wanaokwepa kufanya hivyo, eneo la pili ni eneo la magendo niseme tuu kwamba TRA tupo kwa ajili yakuwahudumia kwa wale wote wanaofanya magendo waache mara moja kwani vyombo vipo na sisi tupo kazini masaa 24 tunawaona, kama mnavyojua magendo yana athari kubwa kwenye uchumi kwahiyo ukiingiza kwenye magendo manake serikali inakosa kodi, ikikosa kodi itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kama mnavyoona kwa mfano sasahivi kuna mvua nyingi madaraja yanakwenda na maji na serikali inatakiwa kuhudumia hiyo miundombinu” Meneja John
Eneo jingine ametaja juu ya kodi kwa piki piki za biashara (bodaboda) kuendelea kujitokeza kulipa kodi ya Sh elfu 65 kwa mwaka na inalipwa kwa awamu nne kwakiwango cha Sh 16200.
Kodi hiyo ni kutokana na mabadiliko ya Sheria ya mwezi Julai 2023 inayowataka wafanyabiashara na wamiliki wa bodaboda kulipa kodi kwa mjibu wa sheria.
Katika hilo Meneja amesema kuwa wameendelea kutoa elimu na mwitikio upo japo waliowengi hawajajitokeza kulipa.
Amesisitiza kwamba kutokulipa kodi kinyume na sheria inaweza wasababishia adha mbalimbali hivyo ni vyema wakalipa ili kuepuka hali hiyo.
Awali amewapongeza wafanyabiashara kwa namna wanavyowiwa na kulipa kodi kwani ndani ya kipindi cha miezi sita imekusanywa zaidi ya Sh Bilioni 30 ukilinganisha na malengo yaliyokuwa yamelengwa ya kukusanya Sh Bilioni 28 kwakipindi hicho.
Amewasihi wafanyabiashara kutumia mamlaka hiyo kwakufika Ofisini kusaidiwa pale wanapokuwa na jambo linalohitaji ufafanuzi.
Ruekaza Rwegoshora ni Afisa elimu kwa umma TRA ameyaelezea mengi yenye kuhimiza ulipaji kodi kupitia nyanja tofauti tofauti zaidi akibainisha wanavyotoa elimu kwa umma kwakutumia njia ya vyombo vya habari, mikusanyiko ya watu hususani majukwaa ya maonyesho na nyinginezo.
Rwegoshora amesema utoaji wa risiti za EFD imekuwa ni moja ya zoezi wanalolivalia njuga muda wote kwani ni eneo muhimu la kusaidia kukusanya kodi ipasavyo.
Mbali na hayo pia wamekuwa wakiwakumbushia kutunza kumbukumbu za manunuzi na mauzo ya bidhaa kwa lengo la kuwawezesha kufanya biashara kwa uaminifu.
Hata hivyo suala la kubadilisha umiliki wa chombo cha moto kutoka kwa mtu mmoja kwenda mtu mwingine limekuwa likihimizwa zaidi maana watu wanapobadili umiliki bila kupitia mamlaka hiyo huweza kuwaletea changamoto kadhaa.
Naye amesisitiza zaidi katika ulipaji kodi bila kushurutishwa pamoja na kushirikiana katika mapambano dhidi ya watu wanaoshiriki biashara za magendo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.