Home Kitaifa TAKUKURU YATATUA KERO MBALIMBALI ZA WANANCHI MKOA WA KAGERA

TAKUKURU YATATUA KERO MBALIMBALI ZA WANANCHI MKOA WA KAGERA

Theophilida Felician. Kagera.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa Kagera imebainisha kuwa katika mapambano yake ya kuzuia na kupambana na rushwa hususani kupitia Programu ya TAKUKURU RAFIKI imefanikiwa kuzitatua kero kadhaa zilizokuwa zikiwakabili wananchi mkoani Kagera.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa TAKUKURU Kagera Pilly alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mwakasege makao makuu ya taasisi hiyo Manispaa ya Bukoba ii leo Tarehe 24 Aprili 2024 kwa amesema kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi yamefanyika mengi yaliyowezesha kuyapata mafanikio ikiwemo ya utatuzi wa kero.

Amezitaja kero zilizowasilishwa na wananchi kuwa nipamoja na kukatika kwa umeme mara kwa mara, uhaba wa maji baadhi ya maeneo , watoto wa shule za msingi kufukuzwa shule bila sababu za msingi, huduma za afya katika zahanati kutokuwa bure kama serikali inavyosema.

Baada ya TAKUKURU kuzipokea kero hizo ilizifikisha kwa mamlaka husika na utatuzi unaendelea vizuri.

Vile vile imesaidia kutatua kero ya kukosekana kwa maji kwa muda mrefu kijiji cha Rwesinga wilaya Kyerwa.

Amefafanua kuwa programu hiyo imezifikia kata 11 jambo liliosaidia kuziibua kero hizo za wananchi.

Katika kipindi hicho pia wamefanya ufuatiliaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo 24 yenye thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 9 na kati ya miradi hiyo miradi 21 ya zaidi ya Sh Bilioni 8 ilibainika kuwa na mapungufu ambayo yalielekezwa kufanyiwa marekebisho ili miradi iendane na fedha zilizotolewa.

Miradi iliyofuatiliwa ni ujenzi wa barabara, zahanati, shule mpya, ujenzi wa matundu ya vyoo, mabweni ya shule mbalimbali za msingi na sekondari.

Baadhi ya miradi iliyobainika na mapungufu ni shule ya msingi Mpango, vyumba vya madarasa Nyabusozi ,B, barabara Biharamulo, ujenzi wa nyumba ya mwalimu Nyakahama shule ya msingi, chuo cha ufundi stadi Veta Misenyi, ujenzi wa mradi wa maji Kyamyorwa, shule ya mpya ya sekondari Makongora, ujenzi wa zahanati mpya ya Kishanda na ukarabati wakituo kikuu cha mabasi Manispaa ya Bukoba.

Kwingineko ameongeza kuwa katika kipindi hicho wamepokea malalamiko 110 kati ya hayo 96 hayakuhusu rushwa na walalamikaji walielimishwa nakupewa ushauri.

Malalamiko 14 yalihusu rushwa nakufunguliwa majalada ya uchunguzi na kati ya hayo 10 uchuguzi umekamilika hatua za kisheria zinatarajiwa kuchukuliwa dhidi ya wahusika na malalamiko 4 uchunguzi unaendelea.

Idara zilizolalamikiwa ni halmashauri malalamiko 49, Fedha 10, ardhi 10 elimu 6, ujenzi 6, afya 7, 61 watu binafsi 21, tarura 3 ushirika 5 polisi 12 na nyinginezo.

Hata hivyo mashitaka 8 yamefunguliwa Mahakamani na kufanya kufikia mashitaka 27 yanayoendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbali mkoani Kagera na mashauri 9 yamefanyiwa maamzi ambapo jamhuri imeshinda yote.

Amevitaja vipaumbele vyao kuwa ni kuendelea kufuatilia ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma, kuendelea kutatua kero za wananchi kupitia Programu ya TAKUKURU RAFIKI.

Amehitimisha akiwahimiza wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuwa waadilifu na wahakikishe fedha zote za miradi zinatumika vizuri kama yalivyo malengo ya serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!