Kaimu Mtendaji Mkuu Bodi ya mfuko wa Barabara Rashidi Kalimbaga amewataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA pamoja na TANROADS kutumia vizuri fedha zinazotolewa na mfuko wa barabara kwa ajili ya utengenezaji wa barabara.
Ameyasema hayo mkoani Morogoro walipokuwa katika uzinduzi wa baraza la wafanyakazi ambapo ameeleza wakala hao wanatakiwa kutumia vizuri fedha hizo kwani matumizi yake ni katika utengenezaji wa barabara tu hasa katika maeneo korofi
Naye Hindu Augossy ambaye ni Katibu mteule wa baraza hilo amewataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo waliyojiwekea.