Home Kitaifa WAZAZI, WALEZI WAPEWA SOMO MALEZI BORA KUPUNGUZA WATOTO WA MTAANI, YATIMA.

WAZAZI, WALEZI WAPEWA SOMO MALEZI BORA KUPUNGUZA WATOTO WA MTAANI, YATIMA.

Na Boniface Gideon, TANGA

Wimbi kubwa la watoto wa mtaani na yatima limekuwa likiongezeka kila siku huku wadau mbalimbali yakiwemo mashirika na taasisi mbalimbali zikijitolea kuwalea watoto,
Ongezeko hilo la watoto wa mtaani pamoja na yatima linatajwa kuwa linasababishwa na Jamii husika kushindwa kutekeleza wajibu wao na kusababisha Watoto kushindwa kupata haki za msingi pamoja na baadhi ya Mila na Desturi ikiwemo lugha za asili.

Akizungumza na wadau mbalimbali Jana wakati wa hafla yakula chakula na Watoto Yatima,
Mkurugenzi wa kituo Cha kulea watoto Yatima cha Goodwill Children’s home Seyyed Idarus,
Alisema wazazi kushindwa kuvumiliana pamoja na ndugu kuwatelekeza watoto pale wanafamilia wanapofariki kumesababisha ongezeko kubwa la Watoto Yatima pamoja na Watoto wa mtaani,

ndugu zangu mliopo hapa na wale mliopo majumbani , niwaambie tu kuwa chanzo kikubwa cha watoto wa mtaani pamoja na yatima inatokana na mafarakano ya wazazi ni chanzo kikubwa cha watoto wa mtaani, lakini pia ndugu na jamaa kushindwa kutimiza wajibu wao pale wazazi au Walezi anapofariki ,hali sio nzuri kabisa”

Aliwataka Wazazi kuvumiliana na kuweka mifumo imara ya malezi ngazi ya familia ili kuweka utulivu pale inapotokea Mzazi au Wazazi wanafariki,

Wazazi tunawaomba Mvumiliane lakini pia wekeni utaratibu mzuri zaidi ambao utasaidia kuongeza utulivu wa Kifamilia,maelewano katika familia yanasaidia sana kuweka mifumo imara ya malezi ngazi ya familia na hata inapotokea Mzazi au Wazazi wanafariki,husaidia Watoto kuendelea kupata utulivu wa Kifamilia kupitia ndugu“Alisema

Kwa upande wake Caroline Bundi mlezi kutoka kituo Cha Watoto Yatima Casade la Joiya kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki, Alisema kazi yakulea Watoto ni kubwa hivyo Jamii inahitaji kushikamana ,

Chukulia Watoto wachache unaowalea hapo nyumbani unavyoangaika nao,sasa sisi wenzenu tunawalea watoto wengi zaidi, Watoto ambao sisi hatujui Mila na Desturi zao, kiukweli ni kazi kubwa inayohitaji moyo, hivyo tunaomba tusaidiane katika malezi ili Watoto hawa wapate haki zao za msingi ili baadae waje waisaidie Jamii” Alisema Caroline

               MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!