Kushinda kesi…Ecc 23.2022
Machi 19, 2024 shauri la uhujumu uchumi Na 23/2022 dhidi ya PAULO NGILORITI TEVELI limeamriwa katika Mahakama ya Wilaya ya Same, mbele ya Mhe Hellen Hozza, likiendeshwa na wakili Suzan Kimaro.
Mshtakiwa ambaye alikuwa Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, ametiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela bila faini.
Mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa mawili:- matumizi mabaya ya mamlaka chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 na kosa la ufujaji na ubadhirifu wa shilingi 8,377,000 / ambazo zilikusanywa na watumishi 3 wa Hospitali ya Wilaya ya Same. Fedha hizi ni za makusanyo ya kila siku kutoka kwa wagonjwa ambazo hakuzipeleka benki kwa kipindi cha Mwaka 2020.
Pamoja na adhabu hiyo mshatakiwa ametakiwa kurejesha fedha alizofanyia ubadhirifu ambazo ni mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Same .