Home Kimataifa WATANZANIA WANAJIVUNIA MIAKA 3 YA UWEZO MKUBWA; NCHIMBI

WATANZANIA WANAJIVUNIA MIAKA 3 YA UWEZO MKUBWA; NCHIMBI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amesema kuwa Watanzania wote kwa ujumla wao wanajivunia uwezo mkubwa wa kiuongozi, anaouonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka 3 ya uongozi wake, ukijidhihirisha kwa namna anavyoiongoza nchi, kwa ajili ya maendeleo ya watu, ustawi wa jamii na kuimarisha utaifa nchini.

Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi wa Kusini, unaoendelea katika siku yake ya pili, kwenye Mji wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe, Jumanne, Machi 19, 2024, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Nchimbi, amesema Chama Cha Mapinduzi pia kinajivunia uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa jinsi anavyoendelea kuiongoza Serikali katika kutafsiri kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025, akisisitiza kuwa CCM na wanaCCM wanamuunga mkono bega kwa bega.

Kabla sijaanza kuwasilisha hapa…kwa ruhusa yako Mwenyekiti wa Kikao, imekuwa kama bahati nzuri zilizogongana leo…naomba niwataarifu Wajumbe wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika kwamba leo ni maadhimisho ya mwaka wa tatu tangu Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposhika Madaraka ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka mitatu iliyopita.

Kwa kweli ninajivunia sana Rais Samia Suluhu Hassan, si kwa sababu tu mimi ni mpigania haki za wanawake, bali kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa uongozi mzuri anavyoendelea kuiongoza nchi yetu ya Tanzania. Kutokana na hilo, Chama Cha Mapinduzi kinajivunia sana uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, na Watanzania kwa ujumla wetu tunajivunia sana kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwezo wake mkubwa ambao ameuonesha ndani yah ii miaka mitatu,” amesema Katibu Mkuu Balozi Dk. Nchimbi.

Dk. Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwahakikishia wajumbe kuwa kutokana na kuwa mwanamajumuia wa kweli wa Afrika, Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati kuimarisha na kuboresha uhusiano wa nchi na vyama rafiki katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na kwamba anafuatilia mkutano huo wa 11 wa Makatibu Wakuu wa vyama hivyo kwa ukaribu, huku pia akiwaomba wajumbe kuungana nae kumtakia kila la heri Mhe. Samia na kumuunga mkono, ombi ambalo lilipokelewa na kukubaliwa na wajumbe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!