Wananchi wa Kata ya Buzilasoga wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wamejitokeza kupiga kura kumuchagua diwani wa Kata hiyo kwenye uchaguzi mdogo.
Aidha uchaguzi huo unafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa Kata hiyo Devid Shilinde (CCM)kufariki dunia.
Vyama nane vimejitokeza kugombea nafasi hiyo ambavyo ni CCM, NLD,ADC, UPDP, ,SAU ,AAFP, CCK, na Demokrasia Makini.
Mkurugenzi wa uchaguzi Jimbo la Sengerema Binuru Shekidele amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri huku wananchi wakifuata taratibu zote za kupigaji kura.