Home Kitaifa ZANZIBAR IMECHANGAMKA KUELEKEA TIGO ZANTEL ZANZIBAR INTERNATIONAL MARATHON

ZANZIBAR IMECHANGAMKA KUELEKEA TIGO ZANTEL ZANZIBAR INTERNATIONAL MARATHON

Baadhi ya Wageni kutoka Mataifa mbalimbali waliokuja kushiriki Tigo – Zantel Zanzibar International Marathon wakiendelea kupata huduma wakisubiri tukio lenyewe litakalofanyika Agost 7 , 2022.


Meneja wa Tigo Zantel Unguja Bwn. Salehe Abdul Salehe ( kushoto ) akizungumza na mmoja wa watakaoshiriki mbio za Tigo Zantel Zanzibar International Marathon 2022 , katika maeneo ya Forodhani Zanzibar Mapema leo hii .


Bwn. Lewis Chadamoyo ambaye ni Meneja wa  Cape Town Fish Market Restaurant iliyopo Forodhani Park Zanzibar akielezea ni kwa jinsi gani ujio wa Tigo Zantel Zanzibar International Marathon umechangia kwa kiasi kikubwa katika biashara yake kutokana na watu kutoka mataifa mbalimbali wanaokuja Visiwani humo kushiriki mbio. 

…………………………………………………….**************************…………………………………..

Na Mwandishi Wetu.

Ikiwa yamebaki masaa kadhaa kuelekea Tigo Zantel Zanzibar International Marathon itakayofanyika kesho Agost 7 , 2022 katika Viwanja vya Forodhani Visiwani Zanzibar , wakazi wa Zanzibar pamoja na wafanya biashara mbalimbali wameelezea utayari wao na kuonyesha kwa namna gani Mbio hizi zilizodhaminiwa na Tigo Zantel zilivyoleta manufaa makubw Katika biashara zao na maisha yao kwa ujumla kutokana na wingi wa watu waliokuja katika visiwa ivyo kushiriki mbio hizo za Kimataifa. 

Akitoa mwongozo Meneja wa Tigo Zantel Unguja Bwn. Salehe Abdul Salehe Amesema kuwa Tigo – Zantel sasa wapo tayari kwa mbio hizo 

” Nipende kuwakaribisha washiriki wote wa Tigo – Zantel Zanzibar International Marathon 2022 na kwa wale ambao washajisajili nawasihi wasogee Catalunya Mall kwa ajili ya kupata Kits zao za kukimbilia ( T- shirt na Namba ) lakini pia kwa wale ambao hawajajisajili  nawasihi wajisajili nafasi bado zipo na mbio zitaaanzia hapa hapa Forodhani saa kumi na mbili alfajiri na kumalizikia hapahapa , karibuni sana na tunaona kabisa Zanzibar imejaa na Washindi Watapata zawadi ya Pesa Taslim kama ambavyo tumetangaza katika kurasa zetu za Mitandao ya Kijamii , Karibuni sana kwa pamoja Tushiriki Tigo Zantel Zanzibar International Marathon 2022 ” Alimalizia .

Kwa upande wao Wafanya biashara mbalimbali ndani ya Visiwa vya Zanzibar akiwemo  Lewis Chadamoyo  Restaurant manager Cape Town Fish Market iliyopo Forodhani , Bi. Purity Warioba Meneja Masoko Golden Tulip Zanzibar na Seleman Bronso Dereva Tax , kwa nyakati Tofauti tofauti wameelezea ni kwa namna gani Tigo Zantel Marathon imeleta watu wengi visiwani humo na jinsi ambavyo ugeni huu umewasaidia kuongeza kipato kupitia huduma wanazozitoa.

Aidha wameongezea kuwa wanaomba Tigo Zantel Zanzibar International Marathon iendelee kufanyika kila mwaka maana uwepo wa mbio hizi ni neema kwa wazawa na zinatangaza utalii wa nchi kwa ujumla , Aidha wamemalizia kwa kusema kuwa Wako tiyari kushiriki Tigo Zantel Zanzibar International Marathon 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!