Home Afya WANAWAKE KATA YA KITAJI WAPELEKA MAHITAJI KITUO CHA AFYA NYASHO

WANAWAKE KATA YA KITAJI WAPELEKA MAHITAJI KITUO CHA AFYA NYASHO

Na Shomari Binda-Musoma

JUMUIYA ya Wanawake (UWT) Kata ya Kitaji wamewatembelea na kusaidia sehemu ya mahitaji kwa wanawake wanaopata huduma na kujifungua kituo cha afya Nyasho.

Mahitaji hayo yamewafikia wanawake hao ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani inayoadhimishwa kila mwaka machi 8.

Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kitaji Anifa Majura amesema kufika kwenye kituo hicho cha afya ni kuonyesha upendo kwa wanawake walio kwenye changamoto.

Amesema kuwa kwenye maradhi au shida ya uzazi kunahitaji kusaidiwa na kuwa karibu na wenye uhitaji.

Mwenyekiti huyo amesema wanawake Kata ya Kitaji wameamua kuwafikia ili kuwaona na kuwasaidia sehemu ya mahitaji.

“Katika kuelekea siku ya wanawake duniani leo tumetembelea kituo chetu cha afya Nyasho ili kuweza kuwaona wanawake na kuwagusa sehemu ya mahitaji”

“Hii ni michango midogo iliyotolewa na wanawake wa Kata ya Kitaji na tunawashukuru kwa kile walichokitoa kwaajili ya wanawake wenzao” amesema Anifa.

Diwani wa viti maalum manispaa ya Musoma Asha Muhamed amesema kila mmoja anapaswa kuwa sehemu ya wahitaji wengine.

Amesema wanawake Kata ya Kitaji wamekuwa na moyo wa karibu wa kusaidia jamii na mara kadhaa wamekuwa wakijitoa kusaidia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!