-AWAOMBA WANAWAKE KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA 2025
Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Mkoa wa Mara Said Mtanda amewataka wataalam kwenye wilaya na halmashauri zote kuhakikisha wanatumia vyema matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Amesema matumizi mazuri na sahihi yataweza kuisaidia serikali kwenye mipango yake ya kuweza kuwahudumia wananchi.
Akifungua mafunzo ya kupokea matokeo ya sensa yaliyoendeshwa na ofisi ya takwimu ya mkoa wa Mara ( NBS) amesema matokeo hayo yana umuhimu mkubwa kwa taifa.
Mtanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya sensa ya mkoa amesema bila kuwa na takwimu hakuna jambo lolote la maendeleo litakaloendelea.
Katika mafunzo hayo yaliyowashirikisha pia maafisa mipango wa wilaya amewasiitiza kuwa viashiria vya sensa viwe chanzo cha kupanga shughuli za maendeleo.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Agness Marwa ambaye alishiriki mafunzo hayo amesr
“Leo ni siku muhimu ya kupata mafunzo juu ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iliyofsnyika hapa nchini”
“Matokeo haya ya sensa yataisaidia serikali kupanga maendeleo ya wananchi wake hivyo ni muhimu kutumika vizuri” amesema Mtanda.
Akizunguamza pia na wanawake wa mkoa wa Mara katika muendelezo wa kupokea matokeo hayo ya sensa mkuu huyo wa mkoa amewaomba kumuunga mkono Rais Suluhu Hassan kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.
Amesema matokeo ya sensa yanaonyesha wanawake ni wengi kuliko wanawaume hivyo wanayo nafasi ya kumfanya Rais Samia kushinda.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Agness Marwa amesema alipochaguliwa kwenye nafasi hiyo lengo lake ni kuwatafutia wanawake.
Amesema wanawake wa mkoa wa Mara kupata mafunzo hayo ni jitihada zake na sio kila mmoja anaweza kufanya hivyo kuwakumbuka wanawake.
Mbunge huyo amesema ni vyema wabunge na madiwani wa viti maalum kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano katika kuwahudumia wanawake.
Meneja ofisi ya takwimu mkoa wa Mara(NBS) David Danda amesema Rais Dkt.Samia Saluhu Hassan anatoa fedha nyingi kwaajili ya miradi mbalimbali na bila takwimu haiwezi kutekelezwa.
Amesema huwezi kuhudumia wananchi huduma za afya elimu,maji na huduma nyingine bila kuwa na takwimu.