Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda akisalimiana na kuzungumza na Wananchi wa Kasulu Vijijini Mkoani Kigoma.
Akiwa hapo, amesikiliza na kusaidia kuzipatia utatuzi kero na changamoto mbalimbali za Wakazi wa eneo hilo.
Makonda yupo mkoani Kigoma kwa muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.