Home Kitaifa TUITUMIE WIKI YA SHERIA KUPATA MSAADA WA KISHERIA ” JAJI MTULYA”

TUITUMIE WIKI YA SHERIA KUPATA MSAADA WA KISHERIA ” JAJI MTULYA”

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI mkoani Mara wametakiwa kuitumia wiki ya sheria kufika kwenye mabanda uwanja wa shule ya msingi Mukendo kupata msaada wa kisheria

Wiki hiyo itafunguliwa na mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda januari 27 na kufikia tamati februari 2 huku elimu mbalimbali juu ya sheria ikitarajiwa kutolewa.

Wito huo umetolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Fahamu Mtulya alipokuwa akiizungumzia wiki hiyo.

Jaji Mfawidhi Mtulya amesema lengo ni wananchi wa Musoma na mkoa wa Mara kupata uelewa juu ya elimu ya sheria ili waweze kupata huduma kwa haki , wakati na urahisi zaidi .

Elimu hii haitatolewa Kwa Mahakama pekee bali imezishirikisha taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na jeshi la polisi,TAKUKURU,Uhamiaji na kadharika Ili wawaze kupata ufahamu wa Sheria za taasisi hizi“, amesema.

Amesema licha ya hayo wanaitambulisha taasisi ya Mahakama ili iweze kujulikana vizuri kwa wananchi hapa nchini na kufurahia Katiba tofauti na hapo nyuma na kwamba dhamira yao ni kutoa haki kwa wakati ili wananchi wapate huduma Kwa urahisi Kwa kuwa sio wananchi wote hufika Mahakamani.

Amesema ,kutoa elimu hiyo ya Sheria ya huduma kwa jamii kutarahisisha kazi za Mahakama Kwa kutumia mifumo ya tehema na urekebishaji wa tabia.

Ameeleza kuwa kuna watu wanahitaji kupata uelewa Kwa taasisi ya polisi na katika ofisi za mashitaka kwani Mahakama ya hapa nchini Ina jukumu la kikatiba la kutoa haki.

Amesema kuna mambo mawili wanayojivunia Kwa sasa Katika utekelezaji wa majukumu yao kuwa kila kitu kinafanyika kutumia mfumo wa tehema na wanajitoa kwa jamii Kwa kuwatembelea na kuwapa msaada watu wenye uhitaji.

Mtu anaweza kufungua kesi yake akiwa kokote aliko Kwa kutumia mifumo hii ya teknolijia ,hivyo naombeni wananchi wa Musoma mjitokeze kutumia fursa hii”alisisitiza Jaji Mtulya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!