Home Kitaifa Mwenyekiti mtaa wa Zahanati akemea uharifu unaochangia kuzorotesha shughuli za kijamii

Mwenyekiti mtaa wa Zahanati akemea uharifu unaochangia kuzorotesha shughuli za kijamii

Na Neema Kandoro Mwanza

MWENYEKITI mtaa wa Zahanati Kata ya Pamba Jijini Mwanza Mashaka Nkonyoka ametaka wananchi kuendelea kuwafichua waharifu katika eneo lao kuwezesha watu kufanya shughuli zao za kila siku bila usumbufu.

Nkonyoka aliyasema hayo leo alipokuwa akizungumzia mafanikio waliyopata yaliyowezesha kutatuliwa kwa changamoto ya vitendo vya wizi uliokuwa unatokea kwenye eneo hilo na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo.

Alisema wananchi wakishirikiana kwa pamoja kutatua vitendo viovu katika maeneo yao wanaweza kufanikiwa kwani wanafahamiana vizuri.

Nkonyoka alisema mafanikio hayo wamepata kwa ushirikiano na jeshi la polisi ambao wamekuwa karibu na polisi jamii katika eneo lao kwa muda wote.

Alitoa pongezi pia kwa wananchi katika eneo hilo kwa ushirikiano wanaotoa kwa viongozi wa serikali ya mtaa wao uliowezesha kuwepo kwa amani sehamu hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!