Akizungumza katika zoezi hilo, Mwenezi Makonda amehimiza kupanda miti ilikusudi kujinusuru kutoka kwenye changamoto ukame na mabadiiko ya hali ya hewa kuwa joto zinazosababishwa na mabadiliko ya Tabianchi.
Katika muendelezo wa sherehe ya kumpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumbukizi ya kuzaliwa kwake. Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ameongoza zoezi la Upandaji miti ambalo wameshiriki Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, Wananchi na Wanafunzi kwa pamoja.
Mwenezi Makonda amezitaja baadhi ya faida za upandaji miti zikiwemo kulinda vyanzo vya maji, kuvuta mvua, kuwa makazi ya viumbe hai mbalimbali, kutoa nishati ya kuni, mkaa na kutoa mbao