Home Kitaifa JESHI LA POLICE MKOANI MWANZA LIMEWAKAMATA ZAIDI YA WATUHUMIWA 300

JESHI LA POLICE MKOANI MWANZA LIMEWAKAMATA ZAIDI YA WATUHUMIWA 300

Na Neema Kandoro Mwanza

ZAIDI ya watu 300 wamekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma mbalimbali katika msako unaondelea kufanywa kuzuia uhalifu wa aina yoyote katika eneo hilo.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mtafungwa ameyasema hayo Leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuelezea hali ya usalama katika mkoa huo.

Alisema watu 335 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali ambapo watuhumiwa 133 wamehojiwa na kufikishwa Mahakamani na 202 bado wanaendelea kuhojiwa .

Kàtika msako huo vitu mbalimbali vilikamatwa ikiwa ni pamoja na simu za mikononi zaidi ya 50, dawa za kulevya kama bangi na mirungi.

Kamanda Mtafungwa amepongeza raia wema waliotoa ushirikiano katika kuwezesha kukamatwa kwa wahalifu na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kizalendo ili kutokomeza matukio ya uhalifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!