Na Mwandishi Wetu
Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar,Mahmoud Mohammed Musa(katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo kipya cha huduma kwa wateja zanzibar, pembeni yake kushoto ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Tigo zantel, Mwangaza Matotola, na kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Zantel ,Zanzibar, Aziz Said Ali.
Zanzibar, 24th Januari 2024 – Tigo Zantel inayo furaha kuutangazia umma kwamba imefanya uzinduzi wa Kituo chake kipya cha huduma kwa wateja kilichoboreshwa. Uzinduzi huo unaashiria kufikia hatua muhimu katika visiwa vya Zanzibar ikiwa ni maendeleo makubwa ya mafanikio yaliyopatikana kwa muunganiko wa Tigo na Zantel ikiwemo uwekezaji uliofanyika kuhakikisha huduma zinaendelea kupatikana kwa kiwango cha juu kwa wateja.
Kituo hichi cha huduma kwa wateja kimeimarishwa kutokana na kuwa na teknolojia ya kisasa ikiwemo kulinda taarifa za mteja kwa usalama wa hali ya juu. Kituo hiki kimeunfdwa na kuboreshwa zaidi kwa ambapo kitakuwa kina uwezo wa kukidhi mahitaji ya wateja zaidi ya milioni 1.5 katika visiwa hivi ikiwemo Pemba na kitakuwa kikitoa huduma kwa kiwango cha kimataifa.
Kwa ushirikiano wa mfumo wa USSD/SMS wa ufuatiliaji na upanuzi wa hoja, pamoja na ufuatiliaji wa 100% wa CRM wa kuridhisha wateja, huduma kwa wateja ya Tigo Zantel imepangwa kufikia watu wengi zaidi ikiwemo kufanya kazi muwda wote. Kituo cha huduma kwa wateja kitakuwa kikitoa huduma zetu kila siku kuhakikisha tunatatua changamoto za wateja na kupunguza foleni zisizokuwa za lazima. Vile vile kimeundwa kwa ufanisi mkubwa ikiwemo wateja kujibiwa maswali mbalimbali kwa ufasaha.
Akizungumza wakati wa kukata utepe wa uzinduzi wa kituo hicho, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo-Zantel, Mwangaza Matotola, alisisisitiza alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo ni kuhakikisha wanawafikia wateja wengi zaidi.
Matotola alisema, dhamira yao ni kuhakikisha wanapanua njia za masiliano ambapo tayari wameshawekeza zaidi ya sh. Trilioni moja tangu mwaka 2022.
“Kituo cha huduma kwa wateja kilichoboreshwa ni mfano wa wazi wa ari hii, iliyoimarishwa na mawakala wa kitaalamu wa Kituo cha Simu, wakituweka katika nafasi nzuri ya kutoa huduma bora kwa wateja isiyo kifani. Mpango wetu wa kimkakati wa kuimarisha na kuboresha miundombinu ya mtandao wetu haujatuletea sifa tu ndani na kimataifa, ikiwa ni pamoja na tuzo ya kifahari ya OoklaSpeedtest lakini pia umeinua kwa kiasi kikubwa matumizi ya kidijitali kwa wateja wetu.”
Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Mohammed Musa, alipongeza kampuni hiyo kutokana na uwekezaji wake visiwani Zanzibar.
Alisema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kisasa visiwani humo ikiwemo Tigo Zantel kuongoza sokoni katika kutoa huduma bora kwa wateja.
“Kupitia kituo cha huduma kwa wateja, umma unaweza kutarajia kupokea uzoefu bora zaidi wa huduma kwa wateja, ninawapongeza kwani mmeleta mageuzi katika upande wa mawasiliano, hii itaongeza ufanisi wa huduma kwa wateja kupitia kampuni ya Tigo- Zantel,” alisema.
Matotola alisema TigoZantel itakuwa na uwezo wa kukabiliana na kutatua changamoto za mawasiliano visiwani Zanzibar.
“Mpango huu wa kisasa umeboreshwa kuendana na kasi ya kidijitali nchini Tanzania ikiwemo vijijini. Uwekezaji wetu mkubwa umechochea kuzinduliwa kwa teknolojia ya haraka zaidi ya 5G (1Gbps) na kuboresha tovuti zote hadi 4G kote Tanzania Bara na Zanzibar, Kituo kipya cha simu kilichoboreshwa kitaenda mbali zaidi katika kuongeza uzoefu, ushindani, na kuharakisha mabadiliko ya uchumi wa kidijitali.
“Mpango wetu na mkakati ni kuimarisha na kuboresha miundombinu ya mtandao wetu na kutuletea mabadiliko kimataifa ambapo tunajivunia kupata tuzo ya OoklaSpeedtest, lakini umeinua kwa kiasi kikubwa matumizi ya kidijitali kwa wateja wetu,”.