Na Magrethy Katengu
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya Ziara katika Nchi za Indonesia, Vatican na Norway ikiwa na lengo la kuimarisha Diplomasia Ushirikiano wa Kiuchumi baina ya nchi hizo.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaaam wakati akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amesema Ziara hiyo ataanzia Nchini Indonesia kuanzia January 24 hadi 26 ,2024 ikiwa na lengo la kukuza na kuimarisha Uhusiano wa kidiplomasia na Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Indonesia kupitia sekta ya Kilimo, nishati, Madini, Mifugo, Uvuvi, Uchumi wa Bluu, Elimu, utalii na ulinzi .
Waziri Makamba amebainisha kuwa kibiashara na Uwekezaji Tanzania imekuwa ikiuza nchini Indonesia bidhaa mbalimbali ikiwemo Pamba ,Tumbaku, karanga, kakao, matunda, kahawa, chai, njugu mawe, mbegu za mafuta, hivyo katika uwekezaji Indonesia imewekeza nchini miradi mitano yenye thamani ya shilingi bilion 6.5 katika sekta za kilimo na uzalishaji wa viwanda na ujenzi.
“Tanzani ni Miongoni mwa nchi inayonufaika kielimu na nchi ya Indonesia ambapo nafasi za masomo zinatolewa na serikali hiyo ( Scholaship) iliongezeka idadi na kufikia 200 mwaka 2018 kutoka 106 mwaka 2015 hivyo pia Ziara hii itaimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano wa nchi hizi mbili kwani tunatarajia hati za makubaliano zitasainiwa” amesema Waziri Makamba
Katika hatua nyingine Januari Makamba alifafafanua Ziara ya Rais Nchini Vatican itakayoanza Februari 11hadi 12 ,2024 kufuatia mualiko aliopewa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Francis ambapo dhumuni la ziara hiyo ni kuimarisha Ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican kwani mwaka 2016 Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli , alimwalika Kingozi huyo kuja kutembelea Tanzania hata hivyo haikuwezekana kutokana na sababu za kifaya.
“Rais Dkt Samia Suluhu Hassani akiwa Vaticani atakutana na kufanya mazungumzo na Baba Mtakatifu Francis pamoja na Katibu wa Vatican Mhe Pietro Parolin hivyo Uhusiano kati ya Tanzania ulianza miaka 1960 wakati ambapo Vatican ilianziasha Ubalozi wake hapa nchini na wakati huo kupitia kanisa Katoliki Vaticani imekuwa mstari wa mbele katika kujihusisha na masuala ya kiroho ,kiimani,elimu, bna progaram za kiafya hapa nchini katika maeneo mbalimbali” amesema Waziri
Aidha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani anatarajiwa tena kufanya Ziara ya Kitaifa nchini Norway kuanzia Februari 13hadi 14 ,2024 hiyo ni ziara ya kwanza kwa kiongozi wa Tanzania kutembelea nchi hiyo tangu mwaka 1976 kufuatilia mualiko kutoka kwa Mfalme Herald wa Norway na Malkia Sonja na ziara hiyo inafanyika ikiwa ni miaka 60 tangu kuanziashwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.
Ziara hiyo ya Rais nchini Norway lengo ni kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi biashara na uwekezaji,nishati,kama mafuta na gesi ,elimu na masuala ya kodi na utawal bora pia atashiriki kongamano la biashara kati ya Tanzania na Norway pamoja na kongamano la Nishati la Oslo.
Katika hatua nyingine Tanzania inatarajia kupokea Viongozi kutoka nje ya nchi kuja kufanya ziara Ikiwemo China Naibu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Watu wa China na Mjumbe wa Kamati kuu 20 ya chama cha Kikomunist cha China Mhe Liu Guozhong anatarajiwa kuanza ziara yake Januari 22 hadi 24 ,2024 atafanya mazungumzo na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko .
Waziri Januari Makamba amebainisha pia Ziara ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Cuba nchi Tanzani Mhe Salvador Valdes Mesa ambapo atawasili katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu kuanzia Januari 23 hadi 25,2024 na atakutana na kufanya mazungumzo na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani , Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango Spika wa bunge wa Jamuri ya Muungano Tanzania Tulia Akson na kuzungumza kwa simu na Mhe Dkt Hessein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar.
Pia Rais wa Jamuhuri ya Poland Mhe Andrzej Duda anatarajiw kufanya zira ya kikazi nchini kuanzia Februari 8hadi 9 ,2024 atakutana na kufanya na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dkt Samia Suhuhu Hassani na lengo la ziara hii ni kuendelea kuimarisha uhisiano wa Kidiplomasia baina na nchi zetu .
Aidha Tanzania na Poland zinashirikiana katika miradi ya maendeleo na miundombinu Uhifadhi wanyama pori , Elimu, maji na Usimamizi wa mazingira , Utalii biashara na Uwekezaji na Ushirikiano wa mabunge na ziara inatarijia kuanzisha maeneo mapya Ulinzi, na Usalama , nishatina gesi, madini, usafiri, ulinzi wa mitandao , utamaduni na uchumi wa buluu.
.