Home Kitaifa MAKONDA AMEBAINISHA UWEPO WA HOSPITAL YA RAIS SAMIA WILYANI MUHEZA ITATATUA CHANGAMOTO...

MAKONDA AMEBAINISHA UWEPO WA HOSPITAL YA RAIS SAMIA WILYANI MUHEZA ITATATUA CHANGAMOTO YA HUDMA ZA AFYA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , Itikadi,Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amewabainishia Wananchi wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kuwa Hospitali ya Rais Samia iliyojengwa Wilayani humo tayari imesha anza kutoa huduma ya afya itakayosaidia kutatua changamoto Katika Sekta ya Afya.

Makonda ameyaeleza hayo mara baada ya kumtaka Mkurugenzi wa Muheza kueleza juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo Mkurugenzi alimthibitishia mbele ya Wananchi hao kuwa tayari imekamilika na huduma zinatolewa.

Mkurugenzi huyo amemueleza Makonda kuwa huduma zilizopangwa kutolewa katika hospitali hiyo zimeshaanza kutolewa kwa asilimia 75% na asilimia 25% zilizobaki ni hatua za mwisho wa ukamilishaji wa majengo machache ambayo tayari wameshaombea fedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!