Home Kitaifa MIGOGORO ZAIDI YA 100 YA ARDHI YASIKILIZWA NA KUPATIWA UFUMBUZI WILAYANI BUNDA

MIGOGORO ZAIDI YA 100 YA ARDHI YASIKILIZWA NA KUPATIWA UFUMBUZI WILAYANI BUNDA

Na Shomari Binda-Bunda

KLINIKI ya utatuzi wa migogoro ya ardhi iliyodumu kwa siku 5 wilayani Bunda mkoani Mara imefanikiwa kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi zaidi ya 100.

Akizungumza wakati wa hitimisho ya kliniki hiyo kwenye viwanja vya stend ya zamani mjini hapa,Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Masase Baraka amesema kliniki hiyo imekuwa na mafanikio.

Amesema wamepokea na kusikiliza migogoro hiyo na kuipatia ufumbuzi huku kwa wale ambao tayari kesi zipo Mahakamani wamepewa ushauri wa kisheria.

Baraka amesema kliniki hiyo ilianzishwa na Wizara ya Ardhi kwaajili ya kusikiliza na kuipatia ufumbuzi migogoro itakayo jitokeza.

Amesema migogoro waliyoipokea na kuisikiliza ni ile inayohusu mipaka,kuvamiwa maeneo na fidia kwa ardhi iliyochukuliwa na manispaa.

Kliniki yetu ya hapa Bunda imefanikiwa kwa kuwa wale waliofika tumewasikiliza na migogoro hiyo imepatiwa ufumbuzi”

“Ipo migogoro ambayo imekuja huku ikiwa na kesi Mahakamani wahusika wake tumewapa ushauri wa kisheria kupitia wanasheria” amesema Baraka.

Amesema kwa mkoa wa Mara kliniki hiyo ilizinduliwa novemba 22 mwaka jana na tayari imeshapita kwenye halmashauri kadhaa na kituo kinachofuata ni Butiama baada ya kumaliza Bunda.

Baadhi ya wananchi waliofika kwenye kliniki hiyo wameishukuru serikali kwa zoezi hilo na kuomba kufika hadi maeneo ya vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!